Tigo Tanzania katika hili kweli mnakera!

Tigo Tanzania katika hili kweli mnakera!

mpuko

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
662
Reaction score
552
Salaam wana jamvi.

Mimi ni mtumiaji mzuri na wa siku nyingi wa huu mtandao wa mawasiliano wa tiGO. Lakini ni kwa muda sasa huduma zao zimekuwa mbovu. Unaweza kutuma sms ikachukua siku nzima kumfikia mlengwa, au wakati mwingine isifike kabisa! Kilichofanya niandike hapa ni kukatika katika kwa huduma ya internet. Jana kutwa hatukuwa na huduma hiyo, wakaomba radhi na kuahidi kufidia huo muda. Leo poa mambo ni yaleyale japo leo ni afadhali kidogo kwakuwa inakatika kwa muda na kisha kurudi.
Tafadhali sana tiGO Tanzania tunawaomba rekebisheni kasoro hizo haraka sana. Lasivyo tutawahama!
 
mkuu why unalalamika kutwa nakupiga mayowee wakati hakunaga kubembeleza kama wanazingua unahamia voda airtel si wapo kwani tigo wamekunywesha maji ya benderaaa
 
mkuu why unalalamika kutwa nakupiga mayowee wakati hakunaga kubembeleza kama wanazingua unahamia voda airtel si wapo kwani tigo wamekunywesha maji ya benderaaa

Hapana sio kunyweshwa maji ya bendera, ila ni kuwaeleza ili wajue udhaifu wao wajirekebishe!
 
Wapuuzi hawa ..mimi tangu juzi sina Internet leo wakani text kwamba watanipatia mb 100 eti kwa masaa 24 what for wakati nikiingia kwenye Internet Network inakata?

Same thing msg azifiki kwa wakati na mara nyingine unaweza kupigiwa kwako aionyeshi bt alie kupigia atakwambia simu imeita muda ....inachosha saana
 
Mimi hata hizo 100mb hawajanipa japo nimejibu sms yao!! Hahaa.
 
Na sikuhiz wananyonya bando kwa spidi ya ajabu.
Hivi kweli kuingia kwenye social networks tena kwa muda waweza maliza mb 150?? Tena bila ya kudownload kitu.
Hawa jamaa waiuze tu hiyo kampuni imeshawashinda.
 
wanakera sana jana walinitumia sms ya kunipa 100mb wakanambia nijibu kama nimeipa kumbuka asubuhi walinitumia sms kuwa kuna tatizo na wahandisi wao wanalishughulikia. Nikawajibu bora mngeacha hivyo ilivyokuwa mwanzo maana imekuwa hovyo kabisa sijui lini tutapata mkombozi wa kweli sababu voda nayo yale yale.
 
Na sikuhiz wananyonya bando kwa spidi ya ajabu.
Hivi kweli kuingia kwenye social networks tena kwa muda waweza maliza mb 150?? Tena bila ya kudownload kitu.
Hawa jamaa waiuze tu hiyo kampuni imeshawashinda.

Wamekuwa ni zaidi ya wezi! Kila kitu kwao ni hovyo!
 
Kila mtandao una janjajanja za kuwaibia wateja wake, voda wamepunguza vifurushi vyao vya cheka, internet ukijiunga ya masaa 24 ukitumia kidogo unatumiwa sms umefikia mwisho wa mb1024. Sms hiyo ikiingia mtandao unapungua speed, airtel hivyo hivyo, tigo kwa huku kwetu internet haipatikani tangu zamani labda utumie kwenye hizi kama Nokia c2 hapo utapata japo kwa tabu
 
Back
Top Bottom