mchukiaufisadi
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 546
- 193
Ndugu zangu nimeibiwa Tshs. 10,000 na Tigo-Pesa. Nilitaka kununua umeme wa LUKU kwa njia ya Tigo-pesa. Nikafuata taratibu zote wakanipa na reference number. Baada hapo sikupokea chochote. Nimejaribu kuwa pigia kwa 0713800800 majibu ya muhudumu ni mabaya mno, kwa ukali akanijibu piga 150. Nimekuwa nikipiga 150 inaita haipokelewi kwa zaidd ya dakika 15 zaidi ya mara 7 toka juzi.
Naomba msaada wa nini cha kufanya nikomboe pesa zangu. Kwenda ofisini kwao itakuwa ni sawa na hasara maana mafuta ni zaidi ya lita 7.
Please help
Mimi mwenyewe wameniibia laki moja kwa mtindo huu within 7 days.Nimekwenda ofice zao nachoambulia ni majibu yasiyoridhisha.tigo ni wezi hapana maelezo,nimekwenda kwa wakala kutoa pesa laki mbili,cha ajabu kwangu itoka haikunipa majibu kama imetoka ila imehama na kwa wakala haijafika, ninasumbuana nao leo siku ya tatu,custorme care wanamajibu mabovu sijapata kuona nikiwa kwenye ofisi zao mlimani city anakuja mama mwingine mwenye tatizo kama langu yeye ni elfu 40,wanamuwakia kisha wakampigia wakala na kutoa hela kwenye akaunti ya wakala kwa nguvu ghafra wakala anakuja na hasira akiwambi mmezidi kunitia hasara sikubali hii ni pesa yangu si ya tigo nataka pesa yangu.mambo ni vurugu tu na wizi kwa kwenda mbele