TIGO PESA na LAKEBROKERS wameshirikiana kuniibia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TIGO PESA na LAKEBROKERS wameshirikiana kuniibia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Crucifix, Aug 3, 2012.

 1. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Naamini JF inasomeka sehemu nyingi, naamini pia kuwa kuna wasomaji watanifikishia hii kwa Tigo. Toka tarehe 18 Julai nimetoa pesa kwa wakala akasema eti nimekosea namba. Kila nikipiga simu naambiwa niwe mvumilivu eti wakala hapatikani kwa simu? ref no sio siri ni C0120718.1202.F04425. Baada ya kupiga simu nyingi sasa nimeanza kuwarekori mimi mwenyewe wahudumu wa tigo, jana alikuwa David na akanihakikishia kuwa ameripoti kama kronik issue nisubiri saa 24. Kumbe wahudumu wamewekwa kama masanamu tu na kujibu kama roboti.Hadi sasa sijapata pesa yangu. Leo nimemkuta Clement naye kasema nimpe ref no, nimekataa kwa sababu huu ni uhuni. Nimemwambia anipe David aliyeniahidi jana kuwa hela yangu itarudi, akaniambia leo david yuko off. Pengine hata majina wanabadilisha hawa watu. Nisaidieni wakuu, nitapataje hela yangu. Kuna mtu au namba nyingine zaidi ya hawa ma-robot?
   
 2. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Nimekomaa sasa kapokea Edith, huyu mpole kidogo na aliponiahidi kuwa suala linashughulikiwa kamekuja na kameseji kutoka +800. Ninachokataa ni kusubiri majaaliwa ya mwenyezi kujua kama nitarudishiwa pesa au la? wash.enzi kweli na vitigo vyao.....
   
 3. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  km uko karibu na customer care office ni heri uende mwenyewe kuliko kupiga simu
   
 4. BJBM

  BJBM JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 545
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Hawa tigo wanamatatizo sana chakufanya kama nipesa nyingi nenda tigo makao makuu kawaeleze
   
 5. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Naomba mwongozo, mamlaka ya mawasiliano wanalijua tatizo hili?
   
Loading...