Tigo na vodacom mnaibia wateja. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tigo na vodacom mnaibia wateja.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by samirnasri, Oct 26, 2011.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Leo tarehe 26/10/2011 imekuwa ni siku ya mshangao kwangu. Mishale ya sa nne asubuhi nilinunua muda wa maongezi wa shilingi kupitia tigo pesa lakini kitu cha ajabu nilijibiwa kwamba nyongeza ya salio la sh. 500 imefanyika kikamilifu lakini sikuona pesa yoyote iliyoongezeka badala yake walinikata pesa hiyo lakini sikuambulia kitu. Nilirudia zoezi hilo mara tatu bila mafanikio na kujikuta nikikatwa shilingi 1500 kwenye account yangu ya tigo pesa bila kuongezewa muda wa maongezi. Nilivuta subira nikiamini kuwa baadae wangenitumia salio langu lakini hadi muda huu saa tatu usiku hakuna lolote. Rafiki yangu naye alifanya hivyo hivyo akakatwa sh. 2000 bila kuongezewa muda wa hewani. Nawauliza tigo je huo ndio utaratibu mpya wa kukusanya mapato...Bhati mbaya zaidi customer care wa tigo hawapatikani.


  Kwa upande mwingine vodacom nao leo wamenishangaza. Nilikuwa na muda wa hewani wa maongezi wa shilingi 1100 niaongea kwa muda wa dakika 6 na sekunde 53 na mteja mwingine wa vodacom kujikuta nimekombwa pesa karibu yote na kubakiwa na shilingi 21 tu. Nilipopiga mahesabu nikajiku nimekatwa wastani wa shilingi 2.67 kwa sekunde nikabaki nikijiuliza garama za kupiga simu vodacom kwenda vodacom zimeongezeka lini kwa zaidi ya asilimia 100!!!!???? Baadae niliamua kupiga simu customer care bahati mbaya sikupata majibu ya kuridhisha. Nilijibiwa kwamba inawezekana kuna matatizo kwenye mtandao hivyo nipige baada ya masaa matatu ili waniangalizie. Nasikitika kuna uwezekano mkubwa sana kwamba makampuni ya simu yamekuwa yakitumia mbinu za ujanja ujanja kujikusanyia mapato isivyo halali. Huu ni wizi wa hali ya juu na unapaswa kukemewa kwa nguvu zote.

  Nawasilisha.
   
Loading...