Kila Siku ya mungu hii mitandao imekuwa kero mnatupandishia gharama za vifurushi kila siku kwa kupunguza dakika mfano tsh 499 tulikuwa tunapata dakika 25 na MB 70 Leo imekuwa dakika 20 MB 50 eti kisa smart phone zinatumika sana katika internet mpate faida kuweni na huruma bas wengine hatuna ajira tunatumia kupiga sim Na Internet kutafuta kaz.
Mmekuwa wanyonyaji sana yaan mnatufanya kama misukule tunaumia sana tunajua upepari ndio unaotupeleka hapa cha kushangaza TCRC hawafanyi chochote zaidi ya kuitisha mikutano ya mablock Na vyombo vya habari.
Ewe mungu lirudishe shirika la TTCL lipamue huduma tuachane na hawa wanyonyaji wenye dhuluma kwa kutumia uchache wao.
Hawa jamaa mimi wamenichosha kwenye kile kifurushi cha internet kwa wiki.
Mwanzoni ilikuwa kwa shilingi 6000 wanakupa GB 10 kwa siku 7,sasa hivi kwa sh6000 unapewa GB 2 tu!!
Jana waliniandikia ujumbe kuwa kutuma sms kwenda mtandao wowote ni bure,baada ya bundle kukata nikaona sio vibaya nkitumia ofa yao,lahaulaa!hakuna cha bure wala cha bura,sasa nkawaza waliwashwa nini kunitumia ule ujumbe waliniona poyoyo au?gardem mazafantazi nyie mitandao ya simu nyie...!
haya mambo ni maswala ya kodi zaidi tukomae na serikali yetu. hii kitu nafananiaha na NISSAN MURANO (gari la ndoto yangu) inayouzwa pale japan dola 3,500. lifikishe bongo ukutane na wazee wa TRA uone! huo ni mfano, anyway nimetumia internet ya airtel zaidi ya miaka mitatu nimeanza kutumia ya tigo naona mambo mazuri, najuta kuchelewa
mkuu bora wapandishe bei za kuingiza gar maana ukininua unaweza ukakaa muda bila kununua ila sio gharama za simu ni daily consumption and its cut across for all civilian include poor people like we