Tigo mnatukera na matangazo ya 'caller tunes'

Tigo mnatukera na matangazo ya 'caller tunes'

Android

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2012
Posts
984
Reaction score
1,240
Ukimpigia mtu hapatikani badala ya kujibiwa hapatikani kwanza unasikia huo mwimbo kama tangazo la caller tune, baadaye ndo unajibiwa hapatikani.

Nampigia mtu anaongea na simu nyingine kwanza napigiwa huo mwimbo kama tangazo la caller tune baadage ndo najibiwa mtumiaji yupo busy.


Binafs ninakerwa sana, pumbaav zenu tigo. Watu tuna haraka na stress zetu mtu hapatikani nijibiwe hapatikani basi, kama yupo busy nijibiwe yuko busy. Mnatutia hasira na kutuondolea mood kila nikipiga simu huo wimbo huo wimbo aargggh!

Hata kama ni tangazo si mngekuwa mnamuwekea mtu huo mwimbo kama tangazo la caller tune mara 5 kwa siku muda mwngine ajibiwe kawaida??!!
 
Ni ukweli kabisa jamaa wanakera hauwezi kujua mtu ana haraka gani wao manyimbo ya kijinga km DK 4 yaani huwa nakereka sana sijui hawana ushauri hawa Jamaaa hebu pitieni humu msome maoni ya Wateja wenu nyambafuuu
 
Nilifikiri nipo peke yangu, kumbe tupo wengi tunaokerwa hilo liwimbo lao
 
to be honest hata mi nakwera sana na huu ujinga wao..... unajua simu inaita kumbe mtu hapatikani
 
Kibaya zaidi ni kwamba wamekaa wakafikiri kwa akili zao zilivyo fupi ni kila mtu anapenda kusikiliza miziki haswa kwenye simu,isitoshe wanafikiri kuwa wote wanaopenda mziki wanazipenda pia hizo nyimbo,na mbaya zaidi wanafikiri kuwa kama mtu anaupenda wimbo basi atataka ausikilize saa zote 24/7...nna waswas na uwezo wa kufikiria kwa hao watu wa Marketing.
 
wanatuchanganya, muda mwingine unapiga ukishasikia huo wimbo unajua mtu hapatikani kumbe yupo bize
 
Back
Top Bottom