TIGO mmeniweza: leo bado kidogo mnikosanishe na mpenzi

mamyake

Member
Jan 2, 2014
88
60
Kisa chenyewe kipo hivi..
Asubuhi ya tarehe 17/2 mwaka huu nilimtafuta mpenzi wangu kwenye simu kumjulia hali kwani jana yake alikuwa mgonjwa. Bahati mbaya nilimtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio. Kwa kutumia namba ya Tigo nikamwandikia ujumbe mfupi wa maandishi uliosomeka hivi "Unanitia hofu mylove, are you okay?Please niambie mume wangu". Na nilipokea ujumbe kuashiria kuwa message yangu ilikuwa delivered.

Sasa cha kushangaza, asubuhi ya leo mwenza wangu amepokea ujumbe ule ule niliotuma tar 17/2. Akawa mkali kunihoji message hiyo nilikuwa naituma kwa nani. Nikajieleza kuwa sijatuma message ya namna hiyo siku ya leo ila mwenzangu hakunielewa kabisa. Baadae zikanijia kumbukumbu kuwa niliwahi kuandika message ya hivyo siku za nyuma, nikajieleza ila mwenzangu akasema hajawahi kupata message ya namna hiyo kutoka kwangu. Yaani ilikuwa patashika. Bahati nzuri
sikuwa nimefuta message za zamani nilizowahi kumtumia. Nikaamua kuzipitia na ndipo nikaikuta message ile na nikamtumia screenshot. Ndipo kidogo mpenzi wangu akatulia.

Sasa hapo kama ningekuwa nimefuta message za zamani sijui ningejieleza vipi, maana mwenzangu alikuwa amecharuka hanielewi. Hii mitandao hii.. dah!​
 
Ukipiga hapatikani, usimtumie tena sms.utamkisa bure! Hata hivyo nipe hivyo namba yake nimpe ushauri pia.
 
Back
Top Bottom