Unazidi kuniongezea hasira make sio tigo tu, mimi vodacom wanakata hela kila siku eti wananiwekea redio ya mziki, wanaweza kukata 200 wakasema ni kwa siku 15, hlf utashangaa baada ya siku4 wanakukata tena eti umeunganishwa upya yaani mimi nina hasira na hawa watu ila basi tu maana ndo serikali yetu, juzi mbunge Azani Zungu kaliongea hili bungeni ya kuwa makampuni ya cm ni wezi but mpaka sasa TCRA hawajasema kitu, hawa dili ni moja. Kuna jamaa kanidokezea eti CCM wameshindwa kuwalipa hela walizotumia kuwapromote wakati wa kampeni kwa kusambaza msg za kumkashifu Dk. Slaa, sasa wameamua kujilipa wenyewe.