:redface:Ni furaha ilioje!!!!!:redface:.
Nilikuwa nikiingoja hiyo huduma kwa muda mrefu na sasa yamekuwa. Tigo wanajiunga pamoja na mitandao mingine hasa hawa mahasimu wao Vodacom na Airtel na kukamilisha utatu wa mitandao inayoaminika na kutumiwa zaidi hapa TZ, kwa kutuwekea 3G Tabora.
Nimekumbwa na mshangao:shock: baada ya kuona Modem yangu ikisoma 3G kupitia laini ya Tigo ambayo matumizi yake kwangu yalikoma tangu nifike hapa Tabora mwanzoni 2013 nikitokea DSM ambapo nilikuwa napendelea kutumia Tigo kwa Internet na kunilazimu nibadili msimamo kutoka Tigo 2G kwenda 3G Vodacom pale nilipotia nanga Tabora.
Kwa Tigo kutuletea hii 3G inazidi kutupatia machaguo zaidi wana-internet wa Tabora kuona upi unafaa kwa wakati huo. Kwa hiyo, Hongera Tigo!!!!!!!!!!:nod::israel::bange: