Hivi Shigela ana umri gani kujibizana na mzee Sumaye, tena alitinga mkutanoni na mtoto wake Filbert. Nahisi kama Shigela kachakachua umri vile kwa jinsi alivyokomaa sura. Ila still haimpi uhalali wa kujibizana na mtu aliyeingia CCM toka wakati TANU youth league wakati yeye shigela kaingia kwa kufuata mkumbo na kutafuta maslahi. Hata iweja au iwe mwisho wa dunia Shigela hawezi kuijua CCM kama Sumaye, regardless of the FISADI behind himmimi sikumwelewa shigela hata kidogo,kwanza ameongea kwa kupanic ajabu,utafikiri kalazimishwa!,kama hao ndiyo viongozi wa umoja wa vijana basi ni makopo kabisa,ningependa kujua elimu yake kwani maongezi yake hayana tofauti na makamba!,yaani anaongea kwa kuropoka!naomba kujua hivi ni makosa kukopa?ni dhambi kuwa na mashamba?,kwa kumbukumbu zangu sumaye aliwai kutuhumiwa akaenda mahakamani mwenyewe kufungua kesi na alishinda,naomba leo lowasa na swahiba wake rostam waende mahakamani wakajisafishe!!!!!!!!!!!!
Afu Dogo Carolite imekubali ile mbaya"Sharobaro" anatakiwa akacheze kiduku siasa hajui wala haiwezi au kama vipi ajiunge Saloon kufanyia watu Masaji ndo kazi za Masharobaro Meeen.kumbe yule ndo shigela?
jamaa alikuwa anazungumza kama amewehuka.
Mwenye macho haambiwi "tazama" kwani UVCCM tuliowatazamia kutupatia viongozi wa "kesho" wanaonyesha dalili mbaya kabla hata ya kukabidhiwa mikoba.
Wanazungumzia kuisubiri zamu yao ya kula washibe kama walivyokula wazee wao (Kina Mwinyi, Mkapa, Kikwete, wezi wenzao, vibaka na mafisadi walioinyonya na kuisulubu nchi kiuchumi.
Hawa ni zao la mafisadi, vibakauchumi na wachumia tumbo waliosheheni ndani ya CCM wasio na chembe ya uzalendo. Ndiyo kina Ridhwani, Makamba Jr. na wengine kibao wenye matarajio ya kukabidhiwa mikoba ya uongozi na kuyaendeleza "Mema" ya chama chao. Wanapaswa kuepukwa kama ukoma.
Unajua siasa ni mchezo wa kujipanga katika kila nyanja (kauli, maamuzi, matendn nk) sasa inaonekana hawa jamaa wamejisahau na mkuu kalala!
Kukinusuru kwa faida ya nani?
kuna dogo mwingine ameonekana ITV akimchambua Sumaye kwa hoja zisizokuwa na uthibitisho. Yaani alikuwa anafanya mipasho zaidi na alikuwa anaonekana amepaniki kwelikweli.
dogo anaona ni dhambi sumaye kuchota 50, 000, 000 (hakuna ushahidi though), lakini anasahau kuwa mafisadi wanaowapigia debe walikuwa wanalipwa 152, 000, 000 kwa siku.
CCM kinakufa jamani. Kinajiuwa chenyewe.
Sasa nimeanza kuona kwamba hakuna tena anayeweza kuikoa ccm
Imani ya Chama
- Binadamu wote ni Sawa
- Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake
- Ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru
AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI
(1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja
(2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote
(3) Nitajitolera nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.
(4) Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa.
(5) Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.
(6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.
(7) Nitashjirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu.
(8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.
(9) Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika.
Jamani hayo hapo juu, Malisa, Bashe, Makamba, NK ndio kweli mnayoyasimamia. Mbona mmefilisika kifikra kiasi hicho. Kimsingi sisiem ni msukule, inahitaji kufufuliwa, Yaani imeshakufa kabisa, ipo kuzimu. Subirini muone
Naomba pitia kipengele kimoja kimoja hapo juu, Naomba:gossip:
CCM Imeishakufa. Hawa wanaojiita CCM sio wenyewe.
Chaka-Chuliwa Makalioni