Tibaijuka, umechepuka katika suala la Mji mpya Kigamboni

Tibaijuka, umechepuka katika suala la Mji mpya Kigamboni

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,506
Reaction score
123,819
Anna Tibaijuka,

Umeulizwa maswali mazuri sana kama nilivyoona kwenye taarifa ya habari ya TBC 1 usiku huu, cha kushangaza, hujajibu swali hata moja, iliyobaki ukapiga porojo.

Sasa, maneno ni rahisi sana kucheza nayo, hapa ni maandiko. Ntajaribu kukuuliza maswali uliyoulizwa ili utujibu hapa. Ukishindwa kujibu, basi jijuwe kuwa unadanganya umma.

Nawaomba wana JF waliosikia maswali mengine ambayo sijayaweka, na wao waulize:

1) Umesema watu wanunue hisa, hizo hisa wanunue kwa nani?

2) Umesema kununuwa hisa ni hiyari ya mtu, Jee, kwanini isiwe shuruti kama ina manufaa?

3) Jee, ni nani anauza hisa za Kigamboni?

4) Thamani ya hisa anaweka nani?

5) Thamani ya hisa watazonunua wana Kigamboni, 100% yake ni ngapi?

6) Jee, wataanza lini kununuwa hizo hisa na ziko wapi?

7) Faida ya hisa zao ni nini?

8) Ramani tunayooneshwa majengo na jinsi mji utavyokuwa Kigamboni, ni ya ukweli au ni ya kubuni kuvutia tu wawekezaji?

9) Hizi porojo za Kigamboni, mwanzo wake lini na mwisho wake lini?

10) Jee, kuna mtu yeyote aliyewekeza Kigamboni na kusema ataanza kufanya nini? lini?

11) Jee, wewe unamiliki viwanja Kigamboni, au mwanao, au Mjomba wako au wa karibu yako?


Ukijibu, tafadhali kumbuka kuwa makini na hakikisha kuwa hapa hatutaki porojo wala siasa. Tunataka ukweli.


Kigamboni wamkaba koo Waziri Tibaijuka



tibaijuka.jpg

Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile akizungumza kwenye kikao cha madiwani na watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kilichojadili malipo ya fidia kwa wakazi watakaopisha ujenzi wa mjini mpya wa Kigamboni. Kulia ni Waziri wa wizara hiyo, Prof Anna Tibaijuka. Picha na Rafael Lubava.
​


Na Nuzulack Dausen, Mwananchi


KWA UFUPI
Pamoja na wito huo, viongozi hao walitaka mpango wa Serikali wa kuwataka wananchi kununua hisa za uendelezaji mji huo kwa asilimia 10 ya malipo ya fidia, uwe wa hiari na Serikali isiingilie uamuzi huo.

Dar es Salaam.
Viongozi wa Mji wa Kigamboni wamemtaka Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kuharakisha malipo ya fidia kwa wakazi watakaopisha ujenzi wa mji mpya na kuacha mikutano ya hadhara isiyokuwa na tija.


Pamoja na wito huo, viongozi hao walitaka mpango wa Serikali wa kuwataka wananchi kununua hisa za uendelezaji mji huo kwa asilimia 10 ya malipo ya fidia, uwe wa hiari na Serikali isiingilie uamuzi huo.

Wakizungumza jana katika semina maalumu kati ya Prof Tibaijuka na viongozi wa mji huo, viongozi hao walisema wakazi wao wamechoka kucheleweshewa malipo yao na kwamba hakuna mkutano wa hadhara utakaofanyika kabla ya masilahi kutimizwa.

Diwani wa Kata ya Kibada, Juma Nkumbi alisema tatizo la uendelezaji mji huo lipo wizarani na si kwa wananchi, kwani wakazi wa maeneo ya Kibada na Uvumba walishakubali kupisha ujenzi huo.

"Asilimia 90 ya wakazi Uvumba na Kibada wako tayari na walishafanyiwa tathmini na kupata mrejesho wa fidia zao, lakini sasa ni mwaka na miezi sita hakuna aliyelipwa," alisema Nkumbi na kuongeza:

"Natoa tahadhari... kusubiri sana bila mafanikio ni hatari."

Awali, katika semina hiyo Prof Tibaijuka aliwasihi viongozi hao kuwaeleza wananchi wao umuhimu wa kununua hisa za taasisi itakayowekeza uendelezaji wa mji huo ili wawe sehemu ya wamiliki.

Alisema kuwa hatapenda kuona wakazi wa eneo hilo wakihama mji na kushuhudia watu wa nje wakinufaika na eneo hilo aliloliita "dhahabu" ya miaka ijayo.

"Itapendeza kama wananchi watakubali kukatwa asilimia 10 ya sehemu ya fidia yao ili iwe malipo ya hisa za kumiliki mji huu. Nitaonekana nimeshindwa, iwapo wananchi watachukua fidia na kuondoka kwenye ardhi ambayo itakuwa dhahabu," alisema Prof Tibaijuka.

Hata hivyo, Mbunge wa Kigamboni Faustine Ndungulile alisema suala la hisa liwe hiari na serikali iweke bayana ni taasisi ipi na namna gani itawekeza fedha hizo ili iwapatie faida wakazi hao.


"Waziri naomba uwajibu wananchi masuala hayo na kama hautaweza mimi sitakuunga mkono hata kidogo. Ni lazima wananchi 2800 wanaosubiri fidia zao wayajue haya," alisema.

Ndungulile alionekana kutoridhishwa na sehemu kubwa ya utekelezaji wa mradi wa mji mpya alisema wananchi hao wamechoka na maneno matupu ya serikali bila ya kuwa na fedha za kutosha.

Aliongeza kuwa serikali iweke wazi kama haina fedha za kutosha ili wananchi wajue nini cha kufanya kuliko kuwazuia watu kufanya shughuli zao katika eneo ambalo linacheleweshwa kulipwa fidia.

"Wananchi kwa sasa hawataki tena mikutano ya hadhara bila fedha za malipo…ujio wako waziri hautapokelewa vizuri," alisema Ndungulile na kuongeza;

"Mimi sina ugomvi binafsi na wewe ila tunatofautina namna ya uendeshaji wa huu mradi…mimi nimetokana na wananchi ni lazima nijali masilahi yao."

Kwa nyakati tofauti Prof Tibaijuka amekuwa akikutana na upinzani mkali kutoka kwa wakazi wa Kigamboni ambao wamekuwa wakilalamikia serikali kutojali masilahi yao ikiwamo malipo ya fidia.

Prof Tibaijuka alibainisha kuwa ucheleweshaji wa malipo hayo umetokana na matatizo mbalimbali ya kiutawala na kimfumo pamoja na ukosefu wa fedha na kuahidi kuanza kutoa fidia hizo kwa kuanzia fedha iliyopo. Mpaka sasa alisema kuna Sh9 bilioni kwa ajili ya mradi huo.

Waziri huyo alisema kwa sasa watahakikisha wanawahudumia wakazi wa Uvumba na Kibada ambapo wataanza kuwalipa fidia watu wenye maeneo madogo huku wenye zaidi ya ekari 5 wakisubiri.

Kuhusu taasisi ya kusimamia uwekezaji na hisa za wananchi Prof Tibaijuka alisema: "Mtaalamu elekezi yupo kwenye mchakato wa kuiandaa na namna itakavyofanya kazi na wananchi watajulishwa hapo baadaye.


CHANZO: Mwananchi

 
Pole dadangu KIGAMBONI ishauzwa siku nyingi ina wenyewe kisa mkondo wa MAFUTA baharini hapo ni mali ya MAREKANI amini usiamini
 
cha ajabu anasema than ya ekari moja ni mil 100+ sasa hivi inamaana iyo eka moja ndo watu wakainunulie hisa ama??
istoshe hebu aseme ukweli juu ya kashfa ya kujimilikisha kigamboni je ni kweli yeye ndo mmiliki?

af naskia wale wasweden wake wa barbojohanson wana maekari ya kumwaga huko je kweli haoni aibu?
 
Na anaweza explain why wahaya wengi sasa wamepewa viwanja kigamboni na bagamoyo kipindi hiki kifupi tu toka apewe wizara?
na kwann thaman ya ardhi kigamboni iwe kubwa kuliko maeneo mengine ambayo ni satellite cities mfano eneo la kibamba
 
Pole dadangu KIGAMBONI ishauzwa siku nyingi ina wenyewe kisa mkondo wa MAFUTA baharini hapo ni mali ya MAREKANI amini usiamini

Haya maswali ni kwa Anna Tibaijuka, kama unaweza yajibu, kama huwezi kaa kimya.

Kama unajuwa Kigamboni imeuzwa, weka ushahidi, kama hauna, hatutaki porojo.
 
Last edited by a moderator:
haya masswali ni kwa anna tibaijuka, kama unaweza yajibu, kama huwezi kaa kimya.

Kama unajuwa kigamboni imeuzwa, weka ushahidi, kama hauna, hatutaki porojo.

pole najua ulitoa hela zako kutaraji kupata kiwanja kigamboni, jamvini mada hujadiliwa kama unamtaka anna tibaijuka ofisi yake iko wazi kamuulize pale wizarani akujibu uso kwa uso ila najua huna uthubutu huo wa kumtokea ndo umekuja malizia hasira zako jamvini acha tukupe za uso
 
pole najua ulitoa hela zako kutaraji kupata kiwanja kigamboni, jamvini mada hujadiliwa kama unamtaka anna tibaijuka ofisi yake iko wazi kamuulize pale wizarani akujibu uso kwa uso ila najua huna uthubutu huo wa kumtokea ndo umekuja malizia hasira zako jamvini acha tukupe za uso

Hapana, sijatoa pesa zangu na huko unakosema "najua", huo ni uongo.
Anna Tibaijuka ni member wa JF, na maswali yalikuwa public na hapa ni public. Anaweza atajibu, la hawezi atakimbia na hatojibu.

Sku nikitaka kwenda ofisini kwake ntakwenda na hatoweza kukataa kuniona, akitaka asitake, mimi ni zaidi ya Taher Muqaddam, akisoma hilo jina anaelewa nnaongea nini. Kumbuka hilo.
 
Last edited by a moderator:
hapana, sijatoa pesa zangu na huko unakosema "najua", huo ni uongo.
anna tibaijuka ni member wa jf, na maswali yalikuwa public na hapa ni public. Anaweza atajibu, la hawezi atakimbia na hatojibu.

Sku nikitaka kwenda ofisini kwake ntakwenda na hatoweza kukataa kuniona, akitaka asitake, mimi ni zaidi ya taher muqaddam, akisoma hilo jina anaelewa nnaongea nini. Kumbuka hilo.

kama alishindwa kujibu bungeni hapa atakuja tusubiri aje kama ana majibu
 
Mwache mama wa watu ajistaafie ubunge. Ninyi mwajua kuwa maccm yameuza kupata fedha za chaguzi nyie mwamshuparia
 
kama alishindwa kujibu bungeni hapa atakuja tusubiri aje kama ana majibu

Kama hajaja basi ajijuwe kuwa ni "bogus". Na kuna siku atajibu, kama si duniani basi akhera.
 
Back
Top Bottom