Tibaijuka= Nitatetea Ubunge Wangu Sijali Ya Escrow!!

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
5,426
Reaction score
3,308
Siku kadhaa tu baada ya rais Kikwete kumfuta kazi Anne
Tibaijuka kama waziri wa ardhi,nyumba na makazi ,kiongozi
huyo amewaambia wakaazi wa Jimbo lake kwamba
hawakumchagua kama waziri bali kama mwakilishi wao wa
bunge, kulingana na gazeti la The citizen nchini Tanzania.
Tibaijuka alipigwa kalamu kutokana na maadili yake
kufuatia kashfa ya akaunti ya tageta escrow ambapo
alipokea sh.billioni 1.6.'' Mungu anayetoa ndiye
aliyechukua jina la mungu libarikiwe alisema tibaijuka
akimaanisha kuwa yule aliyempa kiti hicho cha uwaziri
ndiye aliyekichukua.
Katika kile alichoelezea kama harakati za kukitetea kiti
chake katika uchaguzi wa 2015,Tibaijuka aliwaonya
wapinzani wake wa kisiasa kwamba yeye ndiyo chagua
bora la wapiga kura.
Kulingana na The Citizen kiongozi huyo aliwashukuru
wapiga kura wa eneo bunge lake kwa kumchagua kuwa
mbunge,wadhfa aliodai kumfungulia milango ya kupewa
uwaziri.
''Lazima muelewe kwamba ninyi mulinipigia kura mimi ili
niwahudumie bungeni na sio kama waziri,kwa hivyo
yaliotokea si ndwele tugange yajayo kwa kuwa tayari
kashfa ya escrow imezikwa'',aliwaambia wakaazi wa
Muleba.
Hatahivyo bi Tibaijuka amesema kuwa yuko tayari kufanya
kazi na viongozi wa upinzani waliochaguliwa katika
uchaguzi wa madiwani wa hivi karibuni.

Uongozi Mtamu sana.
 
Kajane kaongo, kajizi, hakana hata chembe ya aibu!!
 
huyu maza anapenda uongozi hadi aibu
_yaani utadhani hajawahi kuwa kiongozi,mbona akina maige walipigwa chini na wakaa tu kimya?
_hana mshauri
 
Ni sababu ya menopause yake ina misbehave ndiyo maana king'ang'anizi
 
Back
Top Bottom