MELEKIZEDECK
Member
- Sep 25, 2012
- 15
- 0
Kitendawili kigumu na ambacho pr Anna tibaijuka hajulikani namna atakavyokitegua kuhusu hatima ya wakazi wa chasimba. kimeendelea kuwatesa wakazi wa chasimba kwa miaka miwili sasa huku kukiwa haukuna jibu lolote nini kinaendelea. kwani matumaini ya wakazi wa chasimba yalijongomea pale walipotegemea kwamba katika bunge waziri angetumia nafasi hiyo kueleza hatima ya mgogoro wao lakini mambo yalikuwa isivyo kwani waziri alishindwa hata kujibu maswali mepesi kutoka kwa mbunge wa kawe Halima Mdee.
Hali hii imefanya Pr Anna Tibaijuka kuwa moja ya watu walioleta matatizo makubwa miongoni mwa wakazi wa chasimba, Kwani kwa mda mrefu wakazi hao walikuwa na umoja sana, lakini waziri alifanikiwa kuusambaratisha umoja huo baada ya kundi moja kukubali mazungumzo na serikali na la pili kugomea mchakato huo kundi lililogomea mchakato huo limekuwa likikosesha amani kabisa katika eneo hilo kwani limeendelea kuendesha vikao usiku kila siku ya jumanne na ijumaa vya siri katika hali ya kupambana na uamuzi wa serikali.
kukaa kimya kwa waziri bila kusema nini kinaendela kumezidi kuwaweka pabaya Mwenyekiti wa mtaa wa Bashaya ndugu Aron na Diwani wa kata ya Bunju Maji safi Kwani kundi hilo pinzani likijiita Mungiki Chini ya uongzi wa ndugu Sakala limekuwa likipanga mashambulizi dhidi ya viongozi hao.