Tibaijuka kitanzini tena sakata la Escrow, TRAB yamuamuru kulipa milioni 586

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
1-2.jpg


Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka amesema yupo tayari kulipa kodi ya mapato ya Sh586 milioni iwapo Mahakama itaamuru hivyo.

Kodi hiyo inatokana na Sh1.617 bilioni alizopewa na mfanyabiashara maarufu nchini, James Rugemalira ambazo zilidaiwa kuchotwa katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Profesa Tibaijuka aliyasema hayo jana baada ya taarifa kwamba Bodi ya Rufani ya Kodi Tanzania (TRAB), imeagiza utekelezaji wa suala hilo ili kutimiza matakwa ya sheria kuhusu mapato nchini.

“Ni kweli ninadaiwa kodi ya Sh586 milioni, ila nimeenda mahakamani kutaka ufafanuzi kama ni halali kufanya hivyo kwa fedha zilizotokana na mchango,” alisema Profesa Tibaijuka na kuongeza “Nilipewa fedha kwa ajili ya shule lakini nadaiwa kama ni kipato binafsi, hivyo nataka Mahakama iseme, ikikubali nitalipa bila shida yoyote.”

Mbunge huyo alifafanua kuwa, anatambua kulipa kodi ni suala la kila mwananchi na anachotaka ni ufafanuzi wa uhusiano uliopo kati ya mapato na kodi.

Alisema lengo ni kutaka kujua iwapo mchango ni sehemu ya fedha zinazostahili kutozwa kodi, bila kujali zimepokelewa zikiwa taslimu au kupitia kwenye akaunti benki.

“Nipo msibani hivi sasa. Watu wanakuja kunipa pole, wengine wanatoka Dar na wasioweza wanatuma michango yao na hapa ndipo nisipoelewa dhana ya kodi kwenye michango. Hii nayo inastahili kuingizwa kwenye mkumbo huo?” alihoji.


Msemaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo alithibitisha kutolewa kwa hukumu hiyo kwenye pingamizi la makadirio aliloliweka mbunge huyo na kueleza kuwa bado anaweza akatafuta haki kwenye mamlaka za juu kama hajaridhika.

“Shauri lake liliamriwa Machi 29 na akatakiwa kulipa kiwango hicho alichokadiriwa,” alisema.

Mbunge huyo wa Muleba Kusini, alitakiwa kulipa fedha hizo baada ya TRAB kutupilia mbali rufaa yake ya kupinga kulipa zaidi ya Sh500 milioni.

Profesa Tibaijuka, Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alikata rufaa hiyo baada ya TRA kumtaka alipe kodi ya mapato Sh586,364,625 kutokana na fedha alizopokea kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited, Rugemalira.

Profesa Tibaijuka ambaye alipokea fedha hizo kupitia akaunti yake iliyopo Benki ya Mkombozi, zilisababisha kuvuliwa uwaziri na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.

Alisema fedha hizo hazikuwa zake binafsi bali zilitolewa msaada kwa Taasisi ya Joha Trust.

Hata hivyo, TRA kupitia kwa Wakili wake, Noah Tito ilisema Tibaijuka anawajibika kulipa kodi hiyo kwani fedha hizo ziliingia katika akaunti yake binafsi.


Chanzo: Mpekuzi Blog
 
Kama fedha ilitoka nje ya nchi.......remittance.....lazima alipe kodi ila kama ilikua hapa hapa ndani hili suala la kodi basi ni jipya

Sina uhakika 100%
 
Hii bado haijaeleweka vizuri, kwamba kila mchango kwa taasisi kama Shule, hospitali, vituo vya yatima nk inatakiwa kukatwa kodi?
Au issue hii ya Tibaijuka ina zaidi ya hapo
 
Hata ukipokea mchango wa ada inabidi ukatwe kodi.
TRA wakate kodi fedha za wanafunzi toka HLSB mara moja ili tuongeze mapato
 
Hata ukipokea mchango wa ada inabidi ukatwe kodi.
TRA wakate kodi fedha za wanafunzi toka HLSB mara moja ili tuongeze mapato
Inafaa tuwajengee tabia ya kulipa kodi watu tangu wakiwa wadogo, hizi fedha za HELSB ni vyema zikakatwa kodi ili vijana waanze mazoea ya kulipa kodi wakiwa wadogo.
 
Hili swala liko wazi. hizo pesa ziliingia kwenye account yake binafsi. Period. Kama zilikuwa za shule kama anavyodai, kwa nini hazikuingizwa kwenye account ya shule?

Nilishasema, watanzania tumezoea kuishi kwa ujanja ujanja......kila kitu tunatafuta mchawi hata kwenye mambo ya wazi. Kipindi hiki cha Magufuli....watu inabidi tubadilike...whether we like it or not. Ni nchi gani unaweza fanya transaction ya pesa hiyo yote usilipe kodi? Mama mpe kaisari halali yake uendelee na maisha yako. Habari ya Keko..si njema...atakusimulia Kitillya.
 
Hapa panahitaji ufafanuzi, nikimtumia baba yangu pesa kwa kuweka kwenye account yake sh 500,000/= itabidi akalipe kodi? TRA mtusaidie maana kama ni hivyo tupo wengi ambao tutadaiwa mimi na ndugu zangu huwa tunachanga kila mwezi kwa wao kuweka pesa kwenye account yangu, ss na mimi itabidi nilipe kodi kisha nami nikiweka kwenye account ya baba nae alipe kodi hapo kidogo mkanganyiko
 
Let's be honest. Huyu mama ni Professor, kwa maana kwamba ana kiwango cha elimu kuliko vyote duniani. Lakini asitufanye watanzania ni wajinga. Anaelewa tofauti ya account binafsi na account ya taasisi. Anazo shule kadhaa zinazo jiendesha kwa account zake, wala account hizo za shule hazina uhusiano na account zake binafsi za pesa yake ya mbonga. Anaelewa kwamba akienda huko Sweden kuomba misaada ya pesa kwa kutumia jina la mama wa kiswidi Barabro Johansen alilo amua kutumia kiujanja ujanja (pengine bila mhusika wa jina kamili kujua) hawezi kutoa account yake binafsi huko ulaya kuwekea hizo pesa za wazungu. Anajua kabisa kwamba usajili wa taasisi yoyote Brela na sehemu zingine unaendana na kufungua account ya taasisi husika, na asingeweza kutumia account yake katika usajili kwa sababu haikubariki. Leo hii anaanza kutuaminisha kwamba ni sawa sawa kutumia account binafsi za wakurugenzi (binafsi au za serikali) kwa malipo yoyote kwa sababu wanaweza kuzipeleka sehemu husika. No, Bw. Rugemarila na yeye mwenyewe walijua kwamba TRA siyo wajinga. It's money laundering na watanzania tunasubiri kuona kama issue itaishia tu na kulipa kodi. Its more that, and we are waiting to see something more happening. You know what I mean, damn! Kama siyo jela, basi angalao lipa hiyo kodi yetu yaishe.
 
Kama kuna mtu kanipa bilioni moja,na inatakiwa nipeleke tra milion 400 kama kodi na nibaki na milion 600,
kaaaazi kweli kweli.

Hizi kodi ni jipu
 
Back
Top Bottom