Captain-Chui
Member
- Dec 11, 2014
- 80
- 49
Historia haikosei. Miaka kadhaa iliyopita kulikuwa na sakata jingine liliitwa Richmond. Bunge likaunda kamati, ikaandikwa ripoti, tuhuma kali zikajitokeza, mheshimiwa Lowasa akaombwa atupishe tuteuwe mwingine. Sasa hivi watu walio wengi Tanzania wanamuomba Mungu usiku na mchana ili Lowasa awe raisi 2015. [hii ni kutokana na un-official kura ya maoni].
Mwaka huu 2014 sakata la Escrow limefumuka, wabunge wamecharuka ikaandikwa ripoti, pesa wamegawana wengine wamebeba kwenye mifuko ya rambo na magunia lakini mama Tibaijuka yeye kwa kujiamini akaziweka kwenye account yake binafsi. Kwa vile account ni ushahidi basi wamemchangamkia mama prof akaombwa atupishe tuteuwe mwingine.
Mwaka kesho 2015, tujiandae ..... Mheshimiwa Lowasa atakuwa Raisi, na Mheshimiwa Tibaijuka atakuwa Waziri mkuu. Sasa, ninyi mlioandika hizo ripoti na kushabikia mtakiona cha mtema kuni.