Tibaijuka ambana mwekezaji Mkinga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tibaijuka ambana mwekezaji Mkinga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 5, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,206
  Trophy Points: 280
  [TABLE="align: left"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody"]Tibaijuka ambana mwekezaji Mkinga
  Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Mkinga; Tarehe: 5th November 2011 @ 11:00
  Habarileo

  WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka amemwagiza
  mwekezaji wa Kampuni ya Arkadia Ltd, Dk. Ezio Copat kuandaa upya mpango mkakati wake wa uwekezaji katika shughuli za kilimo utakaowashirikisha wananchi kabla ya kumilikishwa ardhi katika Halmashauri ya wilaya ya Mkinga.

  Sambamba na hilo Prof.Tibaijuka aliwahakikishia wananchi wa wilaya ya Mkinga kuwa serikali imesitisha mpango wa kumpa ardhi ya hekta 25,189 ambazo katika michakato mbalimbali iliyofanyika awali na wizara hiyo kufuatia kuwepo mkanganyiko wa migongano ya sheria ikiwemo kuzingatia ushauri wa wilaya kwamba haina ardhi ya kutosha kuweza kumpa mwekezaji huyo.

  Kauli hiyo ya Waziri inapingana na barua iliyowasilishwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na barua ya Kamishna wa Ardhi.

  Barua hiyo inaelekeza kuwa serikali imeidhinisha mwekezaji huyo apewe hekta 25,189 sawa na ekari 62,500 kutoka katika vijiji vitano vya wilaya hiyo vya Mavovo, Mwakijembe, Mbuta, Magodi na Mwanyumba.

  Ameyabainisha hayo wakati alipokuwa akizungumza katika kikao cha pamoja kilichojumuisha wananchi wa Kata ya Mwakijembe, uongozi wa wilaya ya Mkinga na mwekezaji huyo kufuatia mgogoro wa ardhi uliokuwa ukifukuta baina ya pande hizo ambao Prof. Tibaijuka alisema serikali haipendi kuona migogoro mipya inaibuliwa katika awamu hii.

  Alisema maagizo hayo yanatokana na ukweli kwamba eneo alilotaka apewe mwekezaji huyo ni
  kubwa ikilinganishwa na mahitaji ya wananchi katika mgawanyo wa ardhi wilayani humo, likiwemo suala la wananchi kukabiliwa na uhaba wa ardhi katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.


  Waziri huyo alisema serikali ipo tayari kumpa mwekezaji huyo hekta 5,386 ambazo atatakiwa kupanda mazao hayo na wakati huo huo, wananchi wajifunze ili walime katika mashamba yao, kisha kumuuzia mwekezaji huyo.

  Hata hivyo aliutaka uogozi wa wilaya hiyo kumpatia orodha ya idadi ya wawekezaji wilayani
  humo ambao wamehodhi maeneo bila kuyaendeleza,
  ili aweze kufuta hati hizo na kuyarudisha
  maeneo hayo mikononi mwa wananchi ili waweze kuyaendeleza kwa kulima mazao ya chakula.

  Awali, Mbunge wa Jimbo la Mkinga Dustan Kitandula, alimtaka waziri kuwawajibisha baadhi ya
  watendaji waliopo wizarani kwake kwa madai kuwa walichangia kuukuza mgogoro huo na hadi kumpotosha Rais Jakaya Kikwete aliyeridhia mwekezaji kupewa eneo hilo wakati wilaya hiyo ya Mkinga haina ardhi ya kutosha.

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Text"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. i

  imosha Member

  #2
  Nov 6, 2011
  Joined: Dec 12, 2007
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Big-up mama tiba!
   
Loading...