Tiba ya Babu: Hatimaye serikali yazinduka?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234

Babu Loliondo abanwa

SERIKALI imesema kuwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila wa Kijiji cha Samunge pamoja na watu wengi waliojitokeza kudai wanatibu magonjwa sugu kwa kuoteshwa na Mungu, wanapaswa kufuata sheria ya Tiba Asilia na Tiba Mbadala namba 23 ya mwaka 2002.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akitoa hotuba yake ya kuahirisha mkutano wa tatu wa Bunge. Alisema kumekuwa na kuibuka kwa watabibu hao wanaodai kuoteshwa na Mungu, ambako kumetokana na kuongezeka kwa kasi kwa magonjwa sugu nchini.

Alitaja masharti hayo kuwa ni pamoja na kujitambulisha kisheria kwa kujaza fomu maalumu ya kujisajili na kuthibitisha usalama wa dawa hiyo katika Maabara za Mamlaka ya Chakula na Dawa na kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Pinda aliwasihi wote wanaotumia dawa hizo kwamba wasiache kujiridhisha kwa kufanya utaratibu wa kupima hospitali ili kuona kama tatizo walilokuwa nalo limekwisha.

Katika hotuba yake, Pinda alisema kuwa tathimini iliyofanywa na watalaamu wa TANESCO na Wizara ya Nishati na Madini mwanzoni mwa mwaka huu, ilionesha kwamba patakuwepo na upungufu wa wastani wa Megawati (MW) 264 za nishati ya umeme katika Mfumo wa Gridi ya Taifa mwaka 2011.

Kwa hali hiyo, alisema wananchi watarajie kuwa na upungufu wa umeme wa wastani wa Megawati (MW)60 katika mwaka wa 2011 na hali hiyo inatokana na mahitaji ya umeme kuongezeka kwa kasi kuliko uwekezaji katika miradi mipya ya kuzalisha umeme.

Pia alizungumzia ajira za walimu ambapo aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri wasiwasumbue Walimu kuwalipa malipo ya Stahili zao mara wanapofika kuripoti katika vituo walivyopangiwa kuanza kazi.

Akizungumzia mchakato wa madiliko ya Katiba, Pinda alisema baada ya Bunge kuurejesha muswada huo kwa wananchi, sasa ni fursa kwa wananchi kuitazama upya katiba yetu.


Chanzo: T. Daima Jumapili

[SIZE="4"

]My take:
Inavyoonekana serikali inaanza kujirudi au kuji-distance kutoka kwa tiba ya Babu.
[/SIZE]
 
Huyu babu afungiwe kabisa halafu ashtakiwe na ikibainika afungwe kwa kusababisha wagonjwa kufa bila uangalizi wakati wakielekea au wakiwa kwake.Ndoto yake ya shetani imeleta usumbufu kwa watu wengi na kwa taifa kwa jumla.
Kama tiba zingekuwa za aina hiyo kuna haja gani ya kuwa na hospitali na vyuo vya afya.
 
Huyu babu afungiwe kabisa halafu ashtakiwe na ikibainika afungwe kwa kusababisha wagonjwa kufa bila uangalizi wakati wakielekea au wakiwa kwake.Ndoto yake ya shetani imeleta usumbufu kwa watu wengi na kwa taifa kwa jumla.
Kama tiba zingekuwa za aina hiyo kuna haja gani ya kuwa na hospitali na vyuo vya afya.
Babu aliwaingiza kingi wakijua kwamba issue zote za maisha magumu na ufisadi wa viongozi ungefunikwa kwa kiasi kikubwa lakini gafla magamba na magome ya dodoma yamekuja juu na kumfunika babu wa loliondo, teh. Na bado, babu atasahaulika kabisa very soon!
 
Kiroho tunasema KIPIMO CHA IMANI, wengi mahudhurio kanisani yameisha kabisa baada ya kujua babu anaponya. Kumbe watu wanaenda church ili wawe healed.

huyu mzee huyu! God have mercy on him!
 
Walokole mmepata pa kujishikiza. Mbona walishapima wakasema haina madhara? Kama siyo tiba mbona wasitangaze hivyo?
 
Nadhani hamkumuelewa vizuri Pinda, maagizo yake yanawahusu hao wengine wanaoibuka kila siku. Kuhusiana na Babu huyo yuko kwenye kiwango cha peke yake; anayebisha amuulize waziri wa afya yaliyompata, tena kutoka ofisina kwa Pinda mwenyewe, alipojaribu kutumia wadhifa wake kuingilia kati matibabu ya Babu.
 
Back
Top Bottom