Threads mtandao mpya tishio kwa twitter

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Vita ya Teknolojia inazidi kushika Kasi Watanzania tukiendelea kujitesa kisa mapenzi, mavazi wenzetu wanazidi kuwa imara.

Meta wametangaza vita dhidi ya Elon musk wa Kampuni ya Tesla.

Threads-1.jpg


Kampuni ya ๐— ๐—ฒ๐˜๐—ฎ wametangaza ujio app mpya inaitwa Instagram threads kama ilivyo Twitter, Facebook , tumblr ambapo watu watakua na uwezo wa ku share picha, videos, pamoja na message kwa marafiki zao.

Uzinduzi wa threads unakuja baada ya mmiliki wa Twitter Elon Musk Toka anunue Twitter ameweka vingepele vingi vigumu kwa watumiaji wake.

images%20(6).jpg


Threads inafanya kazi pamoja na Instagram japo Iko kivyake ukipakua lazima Unganishe na Akaunti yako ya Instagram hivyo followers pamoja na username unaenda nao kwenye app mpya ya threads.

images%20(52).jpg


Pia kuna feature nyingine nyingi tu kama vile
โ€ข uwezo wa kushare, picha, videos pamoja na text message

โ€ข Kuna feature inaitwa story utakua na uwezo wa kuweka stories zako na kukaa ndani ya saa 24hrs kisha kupotea

IMG_20230705_150703_470.jpg


โ€ข kutakua na feature inaitwa short status message kwa ajili ya kutuma jumbe fupi fupi kwenye threads kama ilivyo Instagram note Pia nyingine ni kamera, inbox , status screen nk.

images%20(70).jpg


Jinsi ya Kutengeneza Akaunti kwenye app ya threads ni Rahisi sana

1. Pakua app ya threads an Instagram app kupitia soko la play store na app store

IMG_20230705_150703_441.jpg


2. Tumia taarifa zako za Instagram kutengeneza Akaunti kwenye app ya threads

3. Hivyo itakua Rahisi watu kuweza kukutafuta kupitia app ya threads kupitia jina la Akaunti yako ya Instagram mfano ni bongotech255

IMG_20230705_150703_483.jpg


Itaanza kupatikana siku ya alhamic kwa watu wa marekani kupitia soko la app store.

Tafuta app inaitwa Threads an Instagram App pia watumiaji wa android siku ya jumatatu.

images%20(53).jpg


Unaionaje hii app ni kweli atakua mshindani wa Twitter au bado sana tuachie maoni yako?

images%20(52).jpg
 

Attachments

  • IMG_20230705_150703_470.jpg
    IMG_20230705_150703_470.jpg
    128.3 KB · Views: 7
  • IMG_20230705_150703_483.jpg
    IMG_20230705_150703_483.jpg
    115.4 KB · Views: 7
  • IMG_20230705_150703_456.jpg
    IMG_20230705_150703_456.jpg
    131.5 KB · Views: 10
  • IMG_20230705_150703_441.jpg
    IMG_20230705_150703_441.jpg
    174 KB · Views: 7
Usifananishe Twitter na vitu vya kijinga.

Kidumu chama Cha Mapinduzi
 
Twitter ni affordable sana, unatumia data kidogo sana, ukilinganisha na kampuni ya meta..

Labda na hyo thread iwe nayo affordable kama twitter, na isiwe kama insta
 
Ngoja tupige hesabu tuone kama Threads inaweza kuchukua nafasi ya Twitter kwa maana ya kupata watumiaji wengi zaidi.

Mosi, Instagram inapata 2.3 billion active users kila mwezi.

Twitter 450 milioni kila mwezi.

Hiyo maana yake Meta anauwanja mpana kushawishi hawa 2.3 billion active users wajiunge na mtandao wa Threads. Sasa unaweza ukaona hapa Meta walifikiria hili na wanauhakika watapata watumiaji wengi kwasababu mtaji tayari wanao.

Pili, saa 7 baada ya kuzinduliwa watu milioni 10 wamejiunga na mtandao wa Thread. Hiyo maana yake watumiaji wa social media wamepokea vizuri na nina hakika asilimia kubwa watumiaji wametoka katika hawa 2.3 billion active users.

Kama watumiaji wataendelea kujiunga kwa kiasi hiki kila siku basi itachukua siku 45 tu kufikia idadi ya watumiaji wa Twritter kila mwezi amabo ni 450 millioni.

Lakini hiyo haimaanishi Threads itakuwa na active users 450 milioni sawa na Twitter. Hii jinsi Threads ilivyo na potential kubwa kuchukua nafasi ya Twitter ndani ya miaka michache.


Muhimu pia kuzingatia Threads ina siku 1, Twitter miaka 17 since it first came out.
 
Apps za meta watoto wa mbwa wengi sana, uswahili mwingi
Nili download jana baada ya kama dakika 10 nika ifunga account nikaifuta app, ni Yale Yale ya Instagram, haina mfanano na Twitter hata kidogo itakua ya kawaida kwa sababu imefanana Sana na Instagram lakini kwakua ni mpya ndio maana watu Wana ipakua kwa kasi
 
Nili download jana baada ya kama dakika 10 nika ifunga account nikaifuta app, ni Yale Yale ya Instagram, haina mfanano na Twitter hata kidogo itakua ya kawaida kwa sababu imefanana Sana na Instagram lakini kwakua ni mpya ndio maana watu Wana ipakua kwa kasi
Bora umenisanua mzee, mimi sitaidownload kabisa
 
Back
Top Bottom