PreGE2025 THRDC: Wanahabari wapewe maarifa ya kisheria kuelekea uchaguzi mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umewakutanisha wanahabari 150 kutoka maeneo mbalimbali nchi ili kuwawezesha kuelewa sheria za uchaguzi,maadili ya kazi,usalama kazini na wajibu wao katika kulinda haki za binadamu kipindi cha uchaguzi mkuu ujao wa Oktoba 2025.

Akizungumza Mei 2,2025 wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika Jijini Dar es salaam Mratibu wa THRDC Wakili Onesmo Olengurumwa,amesema ni muhimu wanahabari wakapewa maarifa ya kisheria ili waweze kuripoti habari za uchaguzi kwa weledi,usalama na bila upendeleo.

Aidha ametoa wito kwa vyama vya siasa,taasisi binafsi,serikali na wadau wengine wa uchaguzi kufanya majadiliano ya kitaifa kuhusu mageuzi ya mfumo wa uchaguzi ili kupunguza malalamiko hasa kutoka kwa vyama vya upinzani kuhusu kutokuwepo kwa usawa na uaminifu katika mchakato wa uchaguzi.

Mafunzo hayo ambayo pia ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yanayofanyika kila ifikapo Mei 3,yamewaelekeza wanahabari namna ya kuzingatia taratibu za usalama wao binafsi,panoja na uandishi wenye uwajibikaji na kuheshimu kanuni za kitaaluma wakati wa kuripoti kampeni,upigaji kura na matokeo ya uchaguzi.


Source: Safari media
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…