Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 427
- 666
Kufuatia kukamatwa kwa mwandishi wa Habari Dina Maningo, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umesema mwandishi huyo bado hajapatiwa dhamana jambo ambalo wamedai kuwa kinyume cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
Mtandao huo umeeleza kuwa ulitoa maelekezo kwa wakili Amri Linus aliyepo mkoani Mwanza kushughulikia suala la waandishi wawili walioripotiwa kukamatwa na kupelekwa mkoani humo, hata hivyo taarifa yao imedai kuwa hawajapatiwa dhamana.
Katika tamko la kulaani kukamatwa kwa waandishi wa habari, ambalo limetolewa leo June 18, 2024, imeelezwa kuwa leo wakili Linus kwa niaba ya THRDC amefungua kesi Mahakama Kuu masijala ya Mwanza dhidi ya Jeshi la Polisi mkoani Mwanza ili kudai dhamana ya mwandishi Maningo.
Pia Mtandao unatoa wito kwa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kuwaachia mara moja wandishi wa habari Dina Maningo na Constatine Mathias anayedaiwa kukamatwa akiwa mkoani Simiyu na kusafirishwa kupelekwa Mwanza kama ilivyokuwa kwa Maningo aliyedaiwa kukamatwa akiwa Tarime mkoani Mara.
Wito wao umeeleza kuwa waandishi hao wanatakiwa kuachiwa kwani hao wanatoa taarifa tu ambazo Polisi wanapaswa kuzifanyia kazi na sio kuwakamata na kuwakweka kizuizini kinyume cha Sheria.
Aidha Mtandao huo umetoa wito kwa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kuwarudishia waandishi wa habari vifaa vyao vya kufanyia kazi ili kuhakikisha kwamba wasiingie gharama ya kununua vifaa vingine. Jambo ambalo wamedai kuea litawasaidia waandishi hao pia kuendelea kufanya kazi ya kuipasha habari jamii ambayo ndio kazi mama ya mwandishi wa habari.
Vilevile Mtandao umetoa wito kwa Jeshi la Polisi kufanya upelelezi kwa kuzingatia Sheria na Amri Kuu za Jeshi la Polisi (PGO) ili kuhakikisha kwamba haki za waandishi wa habari hazikiukwi kwa makusudi.
Usiku wa kuamkia leo Juni 18, 2024 imeripotiwa kuwa mwandishi wa habari Constatine Mathias wa Uhuru Media mkoani Simiyu alikamtwa na Jeshi la Polisi.
Tamko la Mtandao huo linaeleza kuwa Polisi walikagua nyumbani kwake na wakachukua vifaa vyake vya kazi ikiwemo simu la laptop yake.
Lakini imeelezwa mnamo Juni 13, 2024 mwandishi wa habari na mmiliki wa Dima Online Tv, Dinna Maningo, alikamatwa nyumbani kwake Tarime mkoani Mara na kusafirishwa hadi mkoani Mwanza kwa tuhuma za kutumia nyaraka za siri za Jeshi la Polisi za kesi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Yahaya Nawanda, anayedaiwa kumlawiti binti wa miaka 21 mnamo Juni 2, 2024 usiku katika eneo la baa ya the Cask, viwanja vya jengo la Rock City Mall.
PIA SOMA
- THRDC yalaani ukamatwaji wa waandishi wa Habari Kanda ya Ziwa