Tafsiri isiyo ya moja kwa moja👇👇
Kutana na mdudu mchanga Assassin Bug — kijana wa kivita wa asili. Lakini huyu si wa kujificha. Anavaa aliowaangusha.
Baada ya kuwavamia na kuwanyonya siafu wakiwa hai, huwachukua maiti zao tupu na kuzipanga juu ya mgongo wake kama kinga ya mwili. Moja baada ya nyingine. Mpaka anatembea chini ya mzigo wa maiti unaosogea.
Kwa nini? Kwa sababu siafu ni wakali, na harufu ndiyo lugha kuu katika dunia ya wadudu. Kwa kuvaa siafu waliokufa, huyu mdudu anawachanganya wanyama wanaomwinda na kuficha harufu yake — anajificha ndani ya kifo kilicho wazi.
Haukimbii. Hauombi huruma. Unajenga ngao kutokana na wale unaowaua. Haujifichi. Unatangaza vita.
JAMANI ASILI NI YA KUTISHA 😨