This is Msamvu bus terminal stand Morogoro

Hio ndio stand bora kwa sasa afrika mashariki na kati.

Stand ya ubungo jijini Dsm ambayo ndiyo stand mama kwa Tanzania yenyewe imekuwa kama gofu lilopigwa bomu na mgambo wa Al qaeda katika vita ya Iraq kwa namna ilivyokuwa hovyo kwa kuwa na uchakavu wa kila namna na majengo yaliyochoka sana pale stand ya ubungo
 
Kwakweli Mara ya kwanza kupita pale Msamvu sikuamini kama ni Tz ,nikajisemea moyoni kumbe inawezekana kwakweli stendi ya Msamvu ndio Bora kushinda zote Tz ina mandhari nzuri ,imepangwa vzr na ina utaratibu mzuri wa kuingia na kutoa mabasi na huduma za kijamii zilizoboreshwa.
 
Mkuu ndio unaiona leo?
Halafu pako vzr mpaka security camera zipo, hapana purukushani ya wapiga debe tena,, nitabaki morogoro daima,
 
 
Ni kati ya projet bora kabisa huyo stendi pamoja na moja ipo Tanga imefunguliwa juzi juzi
 
Ni nzuri kuliko stand ya Ubungo au kiwanja cha ndege jiji la Mwanza
 
Inasemekana ndio stand nzuri Tanzania japo huwa nikipita mchana naona pakawaida.
 
Ni nzuri kuliko stand ya Ubungo au kiwanja cha ndege jiji la Mwanza
Unazungumzia Mwanza?Mikoa hii ya Mza na Shinyanga ni ya watu kuvuna na kuondoka.Wamevuna sana huku na kupaacha hovyo halafu unashangaa viongozi wala hawachukui hatua.Labda awamu hii tunaweza kushuhudia angalau mabadiliko kidogo.
Angalia stand ya Shinyanga,ni lami isiyo na kiwango kabisa lakini mamilioni yaliyotumika hapo ndo utachoka!Vyoo utadhani vya shule ya msingi ya porini kabisa!Vichafu utadhani maji hakuna!Huu mkoa nadhani viongozi ni wachawi sana kiasi kwamba hata akija Majaliwa sijui kama atawafanya lolote!
 
Tatizo la Wabongo ni kutunza vitu, baada ya mwaka sijui itakuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…