Yahya Mohamed: kuna mkanganyiko ambao bado wengi wetu hatujauelewa, kuna wengine kutoka TCRA wanasema kua ukishakua na king'amuzi chako basi wenye king'amuzi wanapaswa kuonyesha chaneli za stations tano bure yaani hata kama hujalipia utaziona nazo ni ITV, chanel ten, Sta tv, eatv na TBC. Jana ama leo kama sikosei nikamsikia tena mtu kutoka TCRA akisema, wao wana mamlaka ya kushinikiza TBC ya taifa ndio ionekane kwenye king'amuzi chochote ila hizi nyingine inabidi makubaliano yafanyike kati ya TV na warusha matangazo sasa hapa naomba uulize lipi ni sa hihi.
Kama la kwanza ni sa hihi kwa nini kwenye king'amuzi cha Easy TV mtu usipolipia unaona TV mbili tu nazo ni TBC na Star TV , hizo nyingine tatu hazionekani mpaka ulipie.