This Friday on Star TV: TCRA na Changamoto ya Digitali

This Friday on Star TV: TCRA na Changamoto ya Digitali

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Posts
270
Reaction score
317
Salaam wakuu,

Kesho Ijumaa januari 11, 2013 Mjadala Mkuu katika kipindi cha Tuongee Asubuhi utaangazia mabadiliko ya mfumo wa Digitali na changamoto zake kwa watumiaji, Mamlaka ya Mawasiliano Nchini TCRA na Watoa Huduma (Kampuni zenye leseni ya kusambaza vingamuzi CONTINENTAL, BTL, TING, ZOUK, EASY TV, STAR TIMES na wengineo).

Mjadala huu utalenga kujibu hoja za kisera ambazo zinatokana na changamoto zilizowakumba wadau wote katika mfumo huu.

Maswali yatakayoulizwa yatasomwa kesho katika Kipindi.

STUDIO DSM atakuwepo:


  1. Innocent Mungi - Meneja Uhusiano TCRA
  2. Joel Chacha - Mhandisi Masuala ya Utangazaji


Karibuni kwa Mjadala
 
Yahya Mohamed: kuna mkanganyiko ambao bado wengi wetu hatujauelewa, kuna wengine kutoka TCRA wanasema kua ukishakua na king'amuzi chako basi wenye king'amuzi wanapaswa kuonyesha chaneli za stations tano bure yaani hata kama hujalipia utaziona nazo ni ITV, chanel ten, Sta tv, eatv na TBC. Jana ama leo kama sikosei nikamsikia tena mtu kutoka TCRA akisema, wao wana mamlaka ya kushinikiza TBC ya taifa ndio ionekane kwenye king'amuzi chochote ila hizi nyingine inabidi makubaliano yafanyike kati ya TV na warusha matangazo sasa hapa naomba uulize lipi ni sa hihi.
Kama la kwanza ni sa hihi kwa nini kwenye king'amuzi cha Easy TV mtu usipolipia unaona TV mbili tu nazo ni TBC na Star TV , hizo nyingine tatu hazionekani mpaka ulipie.
 
sasa mkuu Yahaya kwa nini mnataka kwenda kote huko na mmeshindwa kuajiri ma technician wa uhakika???hivi hamuoni tatizo mnapokuwa na matatizo ya mitambo kila siku???
 
Kwanza ndugu Yahya itoe hiyo kampuni ya ZUKU maana yenyewe haihusiki na mfumo huo maana ukiizungumzia zuku ni sawa na kuzungumzia DSTV hii ni kwa maelezo ya akina Mungi katika kipindi cha Malumbano ya hoja kupitia Itv,na nikukumbushe kuwa makampuni yaliyopewa leseni ni matatu tu yaani TING,STARTIMES,na BASIC TRANSMISION tu.
Swali langu la kwanza kwa akina Inocent Mungi,Mlikuwa mnafukuzwa na nani hadi kukimbia kuweka deadline ya analogia kuwa 31 dec 2012 hali makampuni mliyoyapa leseni yakiwa hayajajitosheleza kwenye usambazaji wa miundombinu yao?,hamuoni kuwa hiyo deadline mliyokuwa mnaitoa haikuwa inawahusu wananchi bali ilikuwa inawahusu makampuni mliyoyapatia leseni.?
 
Mambo ya msingi ambayo muendasha kipindi anatakiwa apate majibu ya kuelekewa ni; local channels ni bure au za kulipia? Kama local channels ni za bure, lakini wateja bado wanalazimika kulipia, je, wapeleke wapi malalamiko yao? Kuna number ya simu ya kupiga? Na pia adhabu gani watapewa haya makampuni yanayotoza fedha kwa local channels?
 
Vp dstv na loko chanelz?au wao hawahusiki?kesho umuulize huyo jamaa wa TCRA

na lin watazindua startimes morogoro{atoe majibu ya uhakika aache ubabaishaji(tcra)}
 
tutaonaje wakat hata star tv haionekani binafsi natumia star times cjui kama vingamuzi vingine vinaonyesha!!! labda mngepeleka kwenye redio
 
pia tungepata majibu ya maswali kwa mfano dstv mbona local channel hazionekani ina maana ukiwa na dstv ni lazima uwe na kingamuzi kingine??
 
pia kuwe na watu wa dstv kwenye mjadala nao watoe msimamo wao haya mambo ya kuficha kichwa ardhini na kuweka pamba masikioni hayatusaidii??? pia local channel ni bure au??
 
Yahaya mohamed kama vipi ili tupate faida na wengine unganisheni tuwapate kwenye radio free maana ving'amuzi vyenyewe hata havieleweki vinaweza kustuck hata nusu saa na kukuta kipindi kimeisha,hii ni kwa wenye navyo,mimi binafsi sina na sijawahi kuangalia tv toka mwaka huu uanze!!!watujibu ili kupata chanels kama tulivyokuwa analojia tununue ving'amuzi vingapi?
 
Tatizo jingine la msingi katika mchakato huu ni urari wa kibiashara kati ya soko la Ndani na mikataba ya wawekezaji wa kimataifa, Na hapa ndio utamkuta DSTV sasa hayo mengine kwa wachangiaji waliotangulia hapo juu kuhusu DSTV sina nayo hakika sana kama yana uhusiano na nachelea kutouliza mambo yenye kujikanganya katika kipindi. Ila tunayafanyia kazi mpaka asubuhi tutakuwa katika nafasi Njema.

Maswali mengine yamekwishawekwa katika line up ya program na yataulizwa mwanzoni kabisa maw kipidni kwa kuwa yanalenga mada husika moja kwa moja.
 
Mkuu Yahya kuna wakati uliwahi kutujulisha kuwa Star TV itakuwa inapatikana kwenye DSTV.
Wazo hili bado lipo?
 
pia tungepata majibu ya maswali kwa mfano dstv mbona local channel hazionekani ina maana ukiwa na dstv ni lazima uwe na kingamuzi kingine??

Hili la kuhusu dstv kuwa na local chaneli zaidi ya tbc,walishalitolea ufafanuzi kuwa wao sheria inawabana tu kuonyesha television ya taifa tu,na hata kama usipolipia malipo yale ya mwezi tbc utaendelea kuiona tu,kuweka chaneli nyingine za hapa tz ni uamuzi wao,hata zuku na easy tv,hawalazimishwi kuweka chaneli zile tano,ila kwa ting na startimes ni lazima zionekane.
 
Yahya tafadhali ondoa neno dijital na tumia neno la kiswahili rasmi dijit
 
Naomba nimuulize bwana Mungi kwa nini hamkutumia teknolojia ya digitali kwa njia ya Satellite kama zinavyotumia kampuni ya Zuku na Multchoice na hii ingewafikia wananchi wengi kwa muda mfupi? Kuliko hayo matransimita ya teknolojia ya terestial.
 
Umeme huku tupipo haupo sijui kama maswali yangu yamejibiwa. Yahya Mohamed kama maswali yamejibiwa naomba uyaandike hapa
 
Last edited by a moderator:
Saaaaafii kabisa mtaalamu toka Mwanza nakubaliana na wewe moja kwa moja kabisa chaneli zilizopo nyingi unapopitia kwenye tovuti kama za Lyngsat zinazohusika na maswala ya masafa ya matangazo ya chaneli zinazorushwa.Pia hamuoni hamtakuwa mnawatendea haki wote ambao walihitaji vingamuzi japo walifikia kununua hivyo ambavyo si vya kiwango?
 
Back
Top Bottom