Thinking out of the "box" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Thinking out of the "box"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Masantula2012, Jun 26, 2012.

 1. M

  Masantula2012 Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bandungu zangu wanaJF.

  Nimekuwa nikiwaza kila siku na kwa kweli kwa miaka nenda miaka rudi; maana naona tutakako kwenda hakuendeki. Na kimsingi, nashawishika kuwa tutabaki kupiga "Marktime" tu kimaendeleo. Achana na uwezo wetu na raslimali tulizo nazo ambazo kimsingi "Viongozi" wetu (Wanasiasa) wameshindwa kututoa katika lindi hili la umaskini. Hii inanikumbusha ile "Theory ya Viscous Cycle of Poverty". Nahisi hatuwezi kufika popote kwa siasa hizi za sasa ambazo kimsingi "badala ya wanasiasa kusikiliza hoja za wale mbadala, imebaki watu kupeana mipasho tu!!???" Naamini tukiendelea hivi, hatutakaa tukifiri kufika huko tunapotaka wandugu. Mf. Mhe. Mwigulu Mchemba badala ya kujenga hoja, anabakia kujisifu kuwa yeye ni Economist Class One (Principal Economist or what ever). By the way kuwa Economist Class one haimaanishi alifaulu sana na au ana akili sana. What matters is the way you translate your education/ knowhow in the development arena. Sasa huku ni kutupotosha na hatutafika kokote. Angalia kilichotokea huko bungeni ambacho ni kichekesho; yaani badala ya Bajeti kuungwa mkono "Freely" kwa kuwa iko sawa inabidi mawaziri waipigie debe ili kuihalalisha kwa wabunge na kwa wananchi. Na Kimsingi, si kwa hoja ila kwa kuiponda bajeti mbadala ( yaani ile ya Kambi rasmi ya Upinzani). Ikumbukwe "Kibaya chajitembeza na kizuri chajiuza". This is and will not take us anywhere my fellow JF Members. Mfano, Chanzo cha mapato kupitia madini (Dhahabu, Almasi, Tanzanite, Rubby n.k. ukiachilia gesi na mafuta) ambayo kingetutoa hapa tulipo ni utata mtupu. Kumbuka yule "Jasusi" aliyetajwa na Mhe. Hamad Rashid..... Viongozi serikalini hawataki kuyagusa haya maana yanagusa maslahi yao. Sasa ukiachilia mbali kuing'oa serikali iliyopo madarakani kwa nguvu, je hatuwezi kuwa na njia mbadala ya kuijenga nchi yetu??? So I thought of the following:-

  1. Nchi inatakiwa iwe na Mpango mkakati mmoja tu wa miaka kumi hadi Ishirini ambao unaheshimiwa na Rais yeyote au chama chochote kitakachoingia madarakani. Katu usibadilishwe kutokana na utashi au maamuzi ya mtu au kikundi cha watu fulani kwa maslahi yao. Hii iwe ni dira ya taifa na sio Dira/ Ilani ya chama fulani. Sio leo tuna Vision 2025, Juzi tukapewa mpango wa miaka mitano (Commonly as "Mpango wa mpango" kwa maana ya Dr. Mpango), tulikuwa na MKUKUTA, MKURABITA, Mwishowe 'MKUKUBI' etc. Hatutafika kama tutaendelea kuwafurahisha "wakubwa" tu na kuyaweka makabrasha haya kwenye Makabineti yetu tu. Hatutaenda kokote ndugu zangu. We need to be focussed guys!!! Ubinafsi ni Sumu!! Tusiwe mabingwa wa Documents ambazo hazifanyiwi kazi au zinahalalisha ulaji wa watu wachache kama MEMM na MESS.

  2. Tukusanye mapato hayo yaliyoanishwa na waziri wa fedha ipasavyo. Halafu tuweze kuhakikisha kuwa tunakidhi matumizi ya serikali (Kwa bei halali za vitu mf. Bei ya Soda badala ya Sh. 2,000 ya sasa wanayoireflect kwenye budget zao, ikawa angalau sh. 1,000; Chupa ndogo ya maji badala ya sh. 2,000 ikawa ni sh. 1,000 etc. Najua mtauliza hizo bei unazipata wapi?? Ni bei za wazabuni ambayo 10% ni ya maafisa ununuzi na ugavi etc. Tofauti ya sh. 300 toka mia saba ya bei mtaani inatosha kuziba lile pengo la delay ya malipo kwa wazabuni. Maana yake kila kitu kitakua ama nusu ya gharama ya sasa au theluthi mbili tu ya gharama. Maana yake matumizi yake kwa ujumla hayatazidi Tirilioni Tano hadi Sita. Kiasi kinachobaki, ndicho kitumike katika gharama/ bajeti ya maendeleo.

  3. Gharama ya bajeti ya maendeleo itokane na salio la fedha kama nilivyo eleza katika ushauri namba moja. Aidha, ijumishe misaada yote yenye masharti nafuu itoloweyo na wahisani kama ni lazima. Katika kulitekeleza hili, tunahitaji kuwa na vipaumbele vya lazima/ muhimu. Mfano kumalizia ujenzi wa barabara ziunganishazo miji yote Tanzania, Masuala ya umeme, Elimu, Afya na Kilimo na siyo kujenga majengo ya ofisi. Mf. kwanini tuwe na jengo la BOT (Pacha) hali ya kuwa kuna majengo mengi tu ambayo yako underutilised?? Kwanini nyumba wa Gavana BOT ikarabatiwe kwa gharama ya zaidi ya Bilioni za kitanzania?? Ukimaliza sekta moja, unaenda kwenye sekta nyingine mwaka hadi mwaka n.k. Hii habari ya "kufakamia" kila waizara na asasi zake, hatufiki kokote ndugu zangu.

  4. Fedha zote zinazomilikiwa na watu (Hasa viongozi na Wafanyabiashara) zilizohifadhiwa katika mabenki nje ya nchi (Halali au zisizo halali) zirejeshwe nchini (Kwa lazima au kwa utaratibu maalumu) na kuwekezwa nchini katika miradi mbalimbali. Rais anaweza kuwapa "incentives" wafanyabiashara/ viongozi kuwa waje wawekeze nchini including yeye mwenyewe, Mkapa et al. Hii ifanyike kama anavyofanya mwenzake Meles Zenawi (Ethiopia). Ikumbukwe kuwa wanapoziacha fedha nje, wanazifaidisha nchi husika na mbaya zaidi wanapofikwa na mauti, wanaziacha huko bila hata wakati mwingine familia zao kujua. Rejea mfano wa San Abacha, Mobutu, Kanali Ghadafi, Balal et al. Hii inatakiwa kuwa amri endapo mtu atakiuka "incentives" In other words, "Guided Investment". tutatengeneza ajira kwa vijana, uchumi utakuwa na maisha kuboreshwa.

  5. Tuwape kazi maalumu wafanyabiashara wenye uwezo ("Specialisation") kama ilivyofanyika katika baadhi ya nchi za Asia. Mf. Bakhresa endeleza seka ya kutengeneza unga au sekta ya usafirishaji majini (Boats na Meli), Mh. Mengi jikite kwenye sekta ya viwanda vya vinywaji, Mh.Sumaye jikite kwenye sekta ya utengenezaji wa nyama za makopo hapa nchini (Packers), Mh. mkapa jikite kwenye kilimo cha majani ya mifugo + uzalishaji wa ng'ombe wa maziwa n.k. Hawa wawezeshwe na serikali yao na iwape masharti ya kuwekaeza na kufanikiwa katika kipindi cha miaka Mitano hadi Kumi tu. wakirudisha mikopo hiyo wapewe incentives na mpango unaendelea tu. Tutakuwa tumejikwamua kichumi na kujitegemea wenyewe. Tutaweza na tutafika.

  6. Tufanye ubinafsishaji wa sekta chache na maalumu ambazo kweli tunahisi sisi hatuna uwezo wa Kifedha, elimu husika na utaalaam. Unawezaje kufikiria kubinafsisha Reli, Bandari, Shirika la ndege n.k. Huu ni ukosefu wa umakini walahi. Hata hivyo, wanaotuwakilisha wajawe na uzalendo ili kulinda maslhi ya nchi na si vinginevyo. Mikataba mibovu ndiyo chanzo cha uozo unaoendelea. Hebu fikiria Bilioni 315 ziko nje na zimelipwa na makampuni ya madini yanayofanya kazi nchini. Hii ni Rushwa na ndiyo masuala haya yanayofanya viongozi wetu waendelee kupigia chapuo misamaha ya kodi kwenye makampuni ya madini katika bajeti. Shame on you!! Hii ni kwa sababu ya Rushwa.

  7. Siasa za unafiki na unzandiki zipigwe vita. Zikemewe. Watu wajali nguvu ya hoja na siyo Hoja za nguvu. Hivi kuna ubaya gani Mtu akitoa wazo mbadala ambalo ni bora kwa maslahi ya nchi yetu??? Kisa ni mpinzani tu au?? Wasomi wazuri kama Lipumba tunawacha, Dr. Salim, Prof. Luhanga, prof. Baregu, Prof. Shivji n.k???

  ITAENDELEA..

  Mniwie radhi kwa kuwachosha, Ila nilihisi tupige marktime kidogo halafu tuwe na mjadala wa kitaifa kutafakari cha kufanya kwa maslahi ya taifa letu. Maana tukiendelea kumlaumu Rais Kikwete tu, hatutafika. yeye atamaliza uongozi wake, na kutuacha tukiwa na nchi yetu iliyouzwa.

  Naomba kuwasilisha hoja na ntaendelea kuainisha fikra mbadala ambazo zitatutoa hapa tulipo na kutufikisha tunapopatarajia. Mzee Jenerali Ulimwengu, Dr. Kitila Mkumbo, Dr. Slaa, Prof. Lipumba, Mh. Zito, Mh. Mnyika, Mh. Lissu and others, please come on Booooooooooard for the future of our country.

  Wasalaam
   
Loading...