Thinking Aloud: Hongera JF kulisaidia Taifa, "Atakuwa anaingia JF in person na kutusoma!". 2021 let's be more responsible, more strategic

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,599
Wanabodi,

Karibuni katika mada hii ya "thinking aloud" ambayo ni moja ya mada zangu za abstracts za hypothetical situations, kumaanisha ni mada ya kufikirika tu lakini inafikirisha, na sio lazima hiki kitu kiwe ni kweli, au ni sisi JF tumekisababisha, lakini likitokea jambo likasemwa humu, likajadiliwa, kisha vyombo vya maamuzi vikatoa maagizo au kufikia maamuzi kuhusu jambo hilo kwa jinsi ile ile lilivyojadiliwa humu JF, kama zilivyo baadhi ya zile mada zangu za "the voices from within", ambazo japo nyingine huwa hazitokei, lakini nyingine ni za kweli hutokea kweli!, sasa zinapotokea kweli, hata kama the cause sio sisi, lakini kama tumepigia kelele jambo fulani, tukashauri na kisha hatua zikachukuliwa, tuna haki kabisa ya kujipongeza kuwa tulichangia!.

Thinking Aloud ni Nini?

Thinking Aloud ni kufikiri kwa sauti, ama kwa kusema ama kwa kuandika. Kwa kawaida kufikiri kunafanyika kwa mawazo ndani ya ubongo, kwenye part of brain, responsible for thinking ambapo tangu binadamu anazaliwa, ile tu kuvuta hewa ya kwanza baada tu ya kutoka tumboni kwa mama, huo ndio mwanzo wa binadamu kujitegemea, kabla ya hapo, kiumbe huyo akiwa tumboni, kila kitu alimtegemea mama aliyembeba miezi 9.

Kwa vile mimi ni mtu wa ma story, kwa wale walio busy, ama wasio na time na ma story, to cut the long story short, mnaweza kuishia hapa na kujump kule mwisho. Wale wa mastory mnaweza kuendelea hapa
Pregnancy inapotungwa, ile sperm inayokutana Ovum na kutengeneza embryo, ili iweze kupenya ovum na kutunga mimba, ina vitu 3 vikuu
1. Body
2. Powers
3. Life force,

1. Body
Body ni umbo, ile kitu, semi liquid, ambayo ndio responsible kuunda embryo yaani umbo, kiumbe, mwili ambao baadaye ndio kinakuwa na binadamu kuzaliwa, kukua na mwisho hufa

2. Powers
Ile mbegu inayorutubisha yai, ni lazima iwe na nguvu ya uwezo wa kupasua ovum, zinakuwa mbegu millions, kwenye kila mshindo mmoja ila yai usually huwa ni moja, hivyo hizo millions sperms zinashindana kupenya kwenye yai moja, na most powerful with maximum power ndio anapasua na kurutubisha.

3. Life Force
Life force ni uhai, ile mbegu ina uhai ndani yake, ule uhai umetoka kwa Mungu, hauna mwanzo wala hauna mwisho, na hiyo life force ndio the source of life and all the power, na ndio responsible for thinking and all conscious things viumbe tunavyofanya.

Ile mbegu ikishakutana na yai na kufanikiwa kupenya ndiko kutungwa pregnancy kwenyewe na hapo hapo from that moment ndio the beginning of life, lile tendo sio la starehe, lile ni creation for a human being kupewa part of uwezo wa Mungu, God The Creator, kumuwezesha binadamu to be a creator wa viumbe kama Mungu, hiyo life force ndani ya mbegu, ni Omnipotence of God ndani yetu, ni uwezo wa Kimungu ndani yetu, na huu ndio uwezo wa binadamu kufanya miujiza, uponyaji au kufanya the impossibles na kwa vile uwezo huo, kila binadamu ameumbwa nao, hapo ndipo kwenye ile dhana ya Omnipresent of God, ndani yetu, Mungu yuko ndani yetu na ndio maana kwa ma pro-life wote, kutoa mimba ni dhambi, ni murder kama murder nyingine zote, wakati kwa ma pro-choice, like tendo kwao ni starehe tuu, ikitokea conception unplanned, wana just flush as if it's nothing!, ndio maana tunasisitiza, ukifanya kwa lengo la kustarehe tuu na kupata raha na burudani, chukua tahadhari, tumia kinga!.

Katika miezi hiyo 9 ya binaadamu kukua tumboni kwa mama, kiungo kikubwa kuliko vyote na kinachosababisha binadamu kutakiwa kukaa tumboni kwa mama miezi yote 9, ni ubongo, ambao huanza kufanya kazi toka mtoto akiwa tumboni.

Ubongo huo una sehemu 2, sehemu ya kwanza inaitwa motor systems ambayo ndio responsible for body control and coordination, hii hailali 27/7 ya siku zote za uhai wa maisha ya binaadamu, na hii motor section kulala, that is the end of life. Hii motor section ndio responsible for bodily activities zote kuanzia kuvuta hewa, mapigo ya moyo, kusaga chakula, na vitendo vyote vinavyofanywa na mwili wa binadamu bila wewe kuviamuru ikiwemo hoja!. Mtu anaposemwa amekufa, kinachokufa ndio hiki, physical body ambayo iko controlled na medulla oblingata.

Sehemu ya pili ya ubongo ni Cognitive brain, ile sehemu inayotumika kufikiri, kuwaza, kutambua, kuona, kusikia, kufeel, ikihusisha the 5 sense, kuona, kusikia, kufeel, kuonja, na the sixth sense ya kuhisi, hivyo thinking aloud inahusisha the sixth sense ya kuhisi na kuandika ndiko kuhisi kwa sauti. Hii ni astral body, spiritual body, wengine wanaiita soul, huu ndio uhai wenyewe, haufi, hauna mwisho ni eternal. This is where the powers is, the will, the conscious, mawazo, fikra etc.

Hiyo Cognitive part of the brain, huwa inaendelea kufanya kazi kwa masaa mengi hata baada ya the motor part kufa, hivyo watu walio kwenye coma au hata waliokufa miili, clinical dead, bado wanasikia mnachozungumza, mnavyolia, mnavyoaga na wengine brain iko hai hadi mwili unaingizwa 6ft under, ndipo astral body au spiritual body, inaachana na physical body, kwa kuuacha mwili kurudi kuwa mavumbi, na roho kwenda kwenye ulimwengu wa roho, kwa sisi Wakristu Wakatoliki, tukiamini unaingia toharani kuisubiri ile siku ya hukumu ya mwisho ya ufufuko wa miili na uzima wa milele, kwa wenzetu wa imani za Hinduism na Buddhism wanaoamini reincarnation, wanaamini hiyo roho yako inaingia kwa kiumbe mwingine na kuzaliwa upya kwenye after life.
Mada hii nimefikia, by thinking aloud kuhusu the role of JF kwenye maendeleo ya taifa letu, na kujikuta ninatoa hongera kwa JF na wana JF kwa mawazo chanya ambayo yanalisaidia sana taifa, letu la Tanzania, kwasababu kuna mtu, au kuna watu, "Atakuwa Anaingia JF in Person na Kutusoma !", na kisha to make sense of mawazo ya wana JF humu, na kisha kuyafanyia kazi, kwa kuchukua hatua stahiki, hivyo kwa kulijua hili, natoa wito kwa mwaka 2021, sisi wana JF, lets be more responsible, kwa kuwa more focused kwenye baadhi ya mada au hoja zinazo husu maslahi ya taifa, tuwe more focused, more strategically na more critical, using critical thinking, tunamsaidia sana huyu jamaa na kulisaidia sana taifa, ingawa huwa hasemi au hawasemi, lakini wanasoma na kuyafanyia kazi baadhi ya maoni yetu humu na hoja zetu humu, mawazo yetu humu na ushauri wetu humu hivyo baadhi ya vitu tunavyo vipigia kelele humu, hatupigi kelele for nothing, ni tunapiga kelele for something, na ni kweli something is being done.

Kiukweli JF itabarikiwa sana na sisi wana JF pia tutabarikiwa!, big up kubwa sana kwa Mkuu, Maxence Melo na team yake, big up sisi wana jf wote in our totality.

Japo kuna mitandao mingi ya kijamii ambayo inaibua hoja mbalimbali kila dakika kama Facebook, Twitter, Instagram, YouTube, tiktock, LinkedIn etc, hakuna mtandao ambao unafanya mijadala na uchambuzi wa issues kama jf, hivyo kitu kikiibuka Twitter au YouTube, kina pata more weight na momentum kama kitajadiliwa humu JF na matokeo chanya ni kuona mawazo ya wana JF yanavyofanyiwa kazi, hivyo JF kujikuta tunatimiza wajibu wetu kwa ama kulisaidia kulijenga taifa kwa kutoa mawazo constructive kulisaidia taifa, au kuliponya taifa kwa kuangazia madudu yanayofanyika as whistleblowers, na hata kwenye ukosoaji wa viongozi wetu na serikali yetu unaofanywa kwa constructive criticism, unalisaidia taifa. Big Up sana wana JF for this.

Kufuatia kinywaji ninachokata, Joni Mtembezi, ni kikali ila stimu zake ni short lived, ukipiga, huchelewi kuzimika, ila pia stimu hazichelewi kuisha, hivyo zikiisha lazima utaamka, utasikia kiu due to nausea, unapata maji, na ndipo unaendelea kulala the normal sleep. Wakati ukiwa kwenye usingizi wa Joni Mtembezi, Cognitive brain inakuwa at complete rest, relaxed na hakuna hata kuota.

Hivyo nilipoamka usingizi umekata, nikajikuta nashika simu janja yangu na kuperlus mitandaoni, nikaanzia Twitter kuzisoma za moto zilizopakuliwa kutoka jikoni, nikaenda YouTube, nikaenda Facebook, nikaenda LinkedIn na kutembelea several blogs na mwisho nikashuka JF

Nilipoanza kuifikiri hii mitandao nikajikuta hakuna mtandao unakata issues za kitaifa kama JF, na nikiangalia impact ya baadhi ya hoja za nguvu za humu JF zenye nguvu za hoja, nikajikuta nashawishika kuwa hata naniliu mwenyewe in person, atakuwa anaingia humu JF na kutusoma, na kufuatia hoja za humu, zinamuingia na anachukua hatua.

Naomba nisiende kwenye hoja specific na hatua specific zilizochukuliwa kufuatia hoja za JF, maadam hata wenyewe hawasemi, naomba na mimi nisiseme ila sisi baadhi yenu tuliojaliwa jicho la tatu na the sixth sense, tunaona, naomba itoshe kusema kuwa jf we are just doing a very good job, for this country na wahusika wanajua, wanaona, wanasikia na wanazifanyia kazi hoja za JF ikiwemo kuchukua hatua stahiki.
Big up sana kwa JF wote, hata wale watema pumba, maana hata hizo pumba ni chakula cha kuku, mtu anayekula kuku mtamu, huo utamu wa nyama ya kuku unatokana na pumba alizokula!.

Big up sana kwa JF wote, JF is power to reckon with!.

Paskali
 
Mkuu huwezi amini, Kabla ya wale maafisa 22 wa TRA kusimamishwa, mimi ndio nilitoa mwongozo huo hapa hapa JF!!.

Baada ya siku chache wazo limefanyiwa kazi japo wengi waliamini ni kama najifurahisha.

Pili sakata la wakurugenzi, limetokea hapa hapa jukwaani.

Yaani mambo mengi yanayofanyiwa kazi through JF.


#jr
 
Tunao wawakilishi wengi makini bungeni wanatosha kutusemea,na tushukuru Mungu safari hii tumepata wabunge wengi kutoka chama makini Chama Cha Mapinduzi .

ukimuona mtu anakesha Jf kuizungumzia serikali na kuitukana tambua huyo ana interest zake binafsi na hao ndio vibaraka wa mabeberu.

Wengi wao hapa Jf wamekuwa kama mbwa koko wanabweka bweka tu hawana madhara pia tuna wale waliokosa teuzi wanakuja kujificha humu Jf kulalama🤔🤔🤔🤔
 
Alishasema ungekuwa uwezo wake angemtuma sijui malaika gani akazime mitandao, kwake mitandao ni dalili ya uvivu hivyo watu hawafanyi kazi kutwa kucha kwenye mitandao.

Nimependa ulivyochambua kazi za brain, binafsi kwangu hapo ndipo nilipopata somo tamu zaidi, na zaidi ingependeza kama ungeendelea kuelezea part ya incarnation (roho ya mtu aliekufa inavyohamia kwa kiumbe mwingine).
 
JF ni Bunge Mbadala la Tanzania... lazima waje wasome maoni ya wanaowapinga au kuwapa ushauri na namna bora ya kutatua matatizo ya nchi...Huko mbeleni, kutakuwa na mashindano ya kimawazo kati ya bunge tukufu na bunge la JF... na huu msuguano wa mawazo ndio utakao tuletea maendeleo kama taifa...
 
Nini maoni yako kuhusu viboko ? DC anaamua tuchapwe viboko, kazi ya Mahakama ni nini ? Na je naweza kumshitaki DC kwa viboko au kwa kuwa anamuwakilisha Raisi wa nchi basi ana kinga ? Ikumbukwe kabla ya kuja Muzungu tulikuwa hatuna utamaduni wa kuchapana viboko, ukatili huu uliletwa na Muzungu, Nyerere akauchukuwa na kuundeleza, siyo utamaduni wetu, ...
 
Back
Top Bottom