Thiago Silva, kifo kilimfuata Urusi, uhai ulimhitaji brazil

Thiago Silva, kifo kilimfuata Urusi, uhai ulimhitaji brazil

Joined
Jun 10, 2017
Posts
8
Reaction score
14
Muongo mmoja uliopita mwanaume mmoja aliamka asubuhi, ili kuhudhuria mazoezi ya klabu baada ya kukamilisha safari muhimu katika maisha yake, kutoka nchini Brazil hadi nchini Urusi. Isivyo bahati, alishindwa kutokana na maumivu makali kifuani mwake.

Nywele zake za rangi ya nyeusi na sura yake bapa, ilimfanya kuonekana mtanashati haswa katika ujana wake. Mama yake Angella na baba yake, Geraldo Emiliano da Silva walimpa jina la Thiago kwa kuzingatia misingi ya dini ya Kiyahudi.

Hii ilikua ni familia yenye misingi ya kidini na iliyojengwa kiimani haswa. Thiago Silva tangu akiwa kijana alikua akiamini katika dini. Ilitajwa kuwa na imani kali kutokana na baba yake Gerlado.

Kutoka Ureno kwenda Urusi akiwa na umri wa miaka 21, ilikua amekifuata kifo chake kabla ya kuwa hai tena. Alikufa akiwa na miaka 21 na kuanza safari ya mpya ya maisha yake baada ya miezi sita tu tangu kifo chake.

Mnamo mwaka 2005, ikiwa ni siku chache tu baada ya kufika Urusi kujiunga na Klabu ya Dynamo Moscow, aliamka asubuhi akiwa anawahi mazoezini, alihisi maumivu makali sehemu ya kifua chake. Maumivu yaliendelea kupenya kutoka mapafuni hadi kwenye ngozi iliyozifunika mbavu zake.

Kwa jamii za Kiafrika wangelirejea katika imani za jadi. Kwa Thiago Silva ilikua ni imani ya Kiyahudi, aliamini ilikua ni changamoto inayomuandaa kuwa mtu mkuu. Mara zote dhahabu hupitishwa katikati ya tanuli la moto mkali ili kuipata thamani yake halisi.

Kocha wake Ivo Wortmann, alimuwahisha kituo cha afya kwa huduma zaidi. Pembeni yake, alikua ni Isabelle na Angella. Isabelle alikua ni mke wa Ivo Wortmann.

Thiago, alikulia katika mitaa migumu ya Rio de Janeiro, Silva alijifunza kutegemea imani tangu akiwa mdogo. Kipaji chake kilikuwa wazi, lakini safari yake haikuwa rahisi.

Madaktari wa nchini Urusi, waligundua ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB). Kama ilivyo kwa wagonjwa wa Kifua Kikuu, hutakiwa kuanza matibabu haraka, alitumia miezi sita hospitalini, na madaktari walifikiria hata kumkata sehemu ya pafu lake.

Isabelle na Ivo Wortmann, walifikia hatua ya kugombana na madaktari wakishinikiza Thiago Silva asifanyiwe upasuaji wa mapafu. Thiago, alikaa hospitalini kwa miezi sita, maisha yake yakiwa ni sindano, vidonge na dawa za TB.

Maisha yake yalining’inia kwenye uzi mwembamba. Aliambiwa hataweza tena kucheza soka. Alikubali kuachana nalo, lakini mama yake, Angella alimshawishi abadili mawazo na kurudi tena uwanjani.

Kinyume na matarajio ya wengi, Silva alipona kikamilifu na kurudi Brazil kujiunga na Fluminense. Huko, aliibuka haraka kuwa mmoja wa mabeki bora wa Amerika Kusini, hali iliyompa nafasi ya kwenda AC Milan.

Italia, alishirikiana na Alessandro Nesta na kuisaidia Milan kutwaa ubingwa wa Serie A msimu wa 2010-11. Uchezaji wake ulimthibitisha kama mmoja wa mabeki bora duniani.

Mwaka 2012, Paris Saint-Germain walimnunua kwa Euro 42 milioni, akawa beki ghali zaidi kwa wakati huo. Akawa nahodha wao, na kuwaongoza kutawala Ligi ya Ufaransa kwa miaka mingi.

Hata hivyo, ubingwa wa Ulaya uliendelea kuwaepuka PSG, ilikua ni hadithi ya vunjiko la moyo, walivunjika moyo, ikiwemo kipigo cha aibu cha 'Remontada' kutoka Barcelona mwaka 2017.

Akiwa na miaka 35, Silva aliiongoza PSG kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza mwaka 2020, lakini wakapoteza kwa Bayern Munich. Msimu huo huo, alijiunga na Chelsea kwa uhamisho wa bure.

Lakini hata akiwa na miaka ya mwisho ya 30 hadi 40, Silva alizidi kuwa nguzo muhimu, akionesha kiwango cha juu katika Ligi Kuu England.

Baada ya safari ndefu barani Ulaya, Silva alirejea nyumbani Fluminense mwishoni mwa msimu wa 2023/24, na mashabiki 55,000 walimkaribisha kwa shangwe na vigelegele.

Akiwa na miaka 40, wachezaji wengi wangekuwa wamestaafu na kusahaulika. Lakini si Thiago. Alirudi Fluminense si tu kama mchezaji mkongwe, bali kama kiongozi, ishara ya uvumilivu, na dira ya matumaini.

Chini ya uongozi wake, Fluminense walifika nusu fainali ya KOMBE LA DUNIA LA KLABU FIFA 2025.

Na siku atakapoamua kupumzika rasmi, kabati lake la makombe litajaa, na urithi wake kama mmoja wa mabeki bora wa kizazi chake utakuwa thabiti. Lakini labda ushindi wake mkubwa kuliko yote? Kukataa kuruhusu ugonjwa uwe mwisho wa ndoto zake.

JICHO LA TATU
Na Halidi Mtumbuka
(Daktari wa Soka).

20250906_122757.jpg
 
Back
Top Bottom