Theresa May ashinda duru ya kwanza ya uongozi wa Conservative

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Theresa May ameshinda duru ya kwanza ya uchaguzi utakaoamua mrithi wa waziri mkuu wa sasa David Cameron.

Mbio za kumtafuta kiongozi mpya wa chama cha Conservative zilianza baada ya Cameron kutangaza kujiuzulu, baada ya wapiga kura wa Uingereza kuamua kuiondoa nchi yao katika Umoja wa Ulaya. Mwandishi wa DW mjini London Birgitte Maass ameripoti kuwa inaelekea mgombea mwenye utata Michael Gove ameadhibiwa kwa usaliti wake na amekuja katika nafasi ya tatu.

Gove aliamua katika dakika ya mwisho kumpinga mshirika wake Boris Johnson ambaye wengi waliamini alikuwa katika nafasi murua ya kushinda uwaziri mkuu. Tayari wagombea wawili wamejiengua katika kinyang'anyiro hicho, na mshindi atajulikana tarehe 9 Septemba.

Chanzo: DW
 
Back
Top Bottom