Kwa sababu vijana wengi wa wanaCCM leo hawana kazi nje ya chama, Elimu na ujuzi wameshindwa kupata ajira ktk mashirika binafsi na last resort ndio mkombozi CCM na ndio maana wengi wamefunga tera nyuma ya Ridhwan au Nnauye.
Hata wale mawaziri wenye elimu utu uzima umewakurubia kiasi kwamba hawawezi kupata ajira ktk ulimwengu wa leo wakavuta fedha kama wanazovuta serikalini. Kwa hiyo wakifikiria kuikosoa serikali mwajiri wao watapoteza kivunia tumbo. Na wazee wetu wengi wao wanakula pension ya chama (serikali) kumalizia kumi lao. Na wale wenye ujasiri mkubwa kama wa binti yetu hapa, wanaifahamu mifano ya kina Kolimba ambalo linahitaji moyo mkubwa zaidi ya uzalendo..
Kwa hiyo ukichunguza sana utagundua kwamba Upinzani wa CCM unatoka kwa watu waliajiriwa nje ya serikali, watu wenye kujiajiri, wafanyabiashara na kadhalika lakini wale wote wanaotegemea serikali hawathubutu kuonyesha wazi upinzani kwa sababu roho zao ziko ICU mikononi mwa serikali...
Acha kutukana baba zako na wakubwa zako