Noel Shao
Member
- Jan 19, 2017
- 89
- 185
ACT NI CHAMA CHA UPINZANI?
Dunia inatembea katika mhimili wake, mengi yana tokea, sahau kuhusu fainali ya UEFA, puuzia audio note inayo sambazwa kuhusu Freeman Mbowe. Mtakie mzee Ndesamburo alale pepa peponi. Muombe Ben Saanane awe salama alipo.
Katika hayo kuna hili la chama cha Act Wazalendo. Nitaandika kwa mtazamo wangu, ni uchambuzi huru usio jikita katika uzio wowote wa kichama.
Nakumbuka katika watu wa awali walio kishauri chama kuhusu namna ya kujitanua ilikuwa ni mimi na andiko lile lilipokelewa kwa bashasha na viongozi wa ACT Wazalendo. Kwa sasa acha niandike tena katika ukurasa mwingine.
Kwanza nimpongeze Mama ana Mghwira kwa kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro. Prof. Kitila Mkumbo kuwa katibu mkuu wizara ya maji. Wote nawafahamu sina shaka na uwezo na utendaji wao.
Ila napata wasiwasi wa mambo kadhaa.
#1. Je Act Wazalendo ni chama kweli cha upinzani nchini?
[HASHTAG]#Jibu[/HASHTAG]; Ni ndio au Hapana.
Ni ndio kwa sababu wana jiita chama cha upinzani ila hawajui malengo, na maudhui chama cha upinzani katika siasa au kwa makusudi wanahubiri mambo nadhani wasiyo yaishi.
#Ni Hapana.
Kwa uelewa wangu chama cha upinzani ni kupingana, kukosoa na kushauri chama tawala. Na si kushirikiana katika kuandaa viongozi kwa ajili ya chama tawala. Hapa wajuvi wa mambo wanatambua kuna "shaka" hapa.
Uteuzi wa Anna na Prof. Kitila ni dhahiri kuwa ACT ni washirika wamoja wa Ccm. Wanacho kifanya Ccm na ACT ni sawa na kuwa na timu ya mpira,. Timu ya mpira huwa inakuwa na timu A na B. Timu A huwa na wachezaji wenye uwezo Mkubwa, wakati timu B ama ni ya watoto au wachezaji wa viwango vya wa wastani.
Mchezaji anavyo Fanya vizuri katika timu B, au kunapo tokea dharura katika timu A, hupandishwa mchezaji mwenye uwezo na kuwa timu A.
Swali 2. Je! Anna Mghwira alijua alilo kuwa ana lihubiri wakati akigombea nafasi ya urais.?
Jibu; Hapana.
ACT kimejipambua kama chama cha wajamaa ndivyo wanavyo jipambanua hata katiba yao ndivyo inavyo ainisha. Sasa inakuwaje wale walio kuwa na mapambano dhidi ya mfumo wa ubeberu uchwara, Leo hii wana kwenda kuutumikia ule mfumo walio kidhana nao? Chama kile kile kilicho iita serikali ni ya udikiteta uchwara Leo wanakweda kushirikiana? Inatia shaka.
Swali 3.Je, Zitto Kabwe anaridhia haya?
[HASHTAG]#Jibu[/HASHTAG];
Hapa naweza kosa jibu la moja kwa moja. Katika historia ya nchi hii hakuna kijana aliye kuwa na ushawishi kama Zitto Kabwe, alisimama bungeni na kuonyesha kuwa alikuwa against government. Nakumbuka 2013 aliwahi kusimama kidete na Waziri wa ujenzi kwa wakati ule juu ya ripoti ya CAG na kila mtu akamuelewa.
Ni huyu huyu Zitto aliye wahi fungiwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa msimamo wake dhidi ya serikali. Kipindi kile alionekana kuliko hata wakina Lissu na Lema.
Ila unajiuliza tangia awe na chama cha ACT je ni yule old Zitto, new Zitto au ni fallen Zitto?
Haya yanayo tokea katika chama chake anaya ridhia kwa lengo gani? Au ana hujumiwa ili kuvuruga nguvu ya upinzani? Na kama ni kuhujumu upinzani mbona uteuzi upo upande mmoja??
[HASHTAG]#Swali4[/HASHTAG]. ACT kinaweza kupotea katika ramani ya vyama vya upinzani nchini?
[HASHTAG]#Jibu[/HASHTAG]; Jibu ni ndio.
Dunia kote hakuna chama cha upinzani kinacho shirikiana na chama tawala katika kuandaa viongozi. Kuna mambo huweza kushirikiana ila si kama wafanyavyo ACT.
Hebu jenga fikra za haraka, kama Zitto Kabwe akiondoka ACT nini kitafuata? Uhai wa chama utabaki kwa nani? Na ikatokea Ado Shaibu naye akapata uteuzi hatima ya kustawi kwa chama utabaki kwa muasisi gani mwingine? Wenye uwezo na ushawishi wengi wamesha toka, Prof. Mkumbo, Mghwira, Mchage, Moses Machali, Msando, Afande Sele n.k.
Pia jiulize chama kikirudi kwa wananchi kinaenda kujipambunua kwa Sera zile zile au Sera mpya, kuwa wao wanaanda viongozi wa nchi? Hapa tukubaliane katika kutokubalina kuwa watapata upinzani Mkubwa.
Swali 5. Mama Anna Mghwira na Prof. Kitila watabaki kuwa wanachama wa ACT?
[HASHTAG]#Jibu[/HASHTAG];
Hapana. Na jibu hili ni kutokana na katiba ya Ccm na katiba ya nchi. Ukisha teuliwa kuwa mtumishi wa serikali katika political operations moja kwa moja unakuwa ni mwanachama wa Ccm.
Ndimi, Noel Shao.
[HASHTAG]#mjenziWaTanzaniaMpya[/HASHTAG]