"The War We must Loose"

Faru John II

Senior Member
Dec 27, 2016
134
135
(Jicho la Tatu katika Vita dhidi ya Mihadarati)

Hii ndiyo dunia ya Propaganda bwana kama umelala shauri yako. Kuna mbinu moja hutumika na wezi kwa lengo la kuwanasua wezi wenzao katika mtego walionasa baada ya kufanya uharifu mahala. Hii mbinu inakuwaje? Haya tega sikio nikupe uhondo mwanana, baada ya wezi kubaini kuwa mwenzao amenaswa na hawezi kujinasua ktk mtego wa raia wema basi huanzisha mayowe ya mwiiizii! Mwiiizii! Mwiiizii! Wakiyaelekeza katika eneo la jirani na tukio mpaka watakapo jiridhisha mwenzao ameachwa na raia wameelekea kwenye makelele ya mwizi wakidanganywa na baadhi waliojipachika kwenye tukio kumbe ndani ni mbwa mwitu, basi wakishaelekea kwenye makelele wezi huwatoroka na kwenda zao. Sasa, yatupasa kuwa makini na makelele ya Makonda na Swahiba zake yasiwe na lengo la kuwanasua wahusika tukawaona wako safi na tukapoteza uelekeo.

Katika Vita, sio kila vita ni Vita. Kuna vita huanzishwa kwa lengo la kufunika Kombe Mwanaharamu apite. Mwanaharamu huyu akishapita basi mchezo unaendelea kwa speed ile ile (deal as usual). Wakati mwingine huanzishwa Vita ili kuzima vita. Inaweza kuanzishwa vita kwa lengo la kimkakati, mkakati ambao utawafanya baadhi ya watu wasahau kabisa story walizokuwa wakiongea jana na kudakia story mpya ambazo lengo lake hawalifahamu.

Huwezi kufanya zoezi la kuwaondoa Funza chooni utakuwa unapoteza muda, bora ufanye shughuli nyingine. Mazingira ya Tanzania yamekithiri tabia ya Rushwa na Ufisadi uliyokubuhu katika mihimili yote mitatu ya Nchi sio Mahakama, sio Bunge sio Serikali, pote panaharufu mbaya sana ya rushwa na ufisadi. Wewe ni nani mpaka ushinde vita katika mazingira haya? Ukitaka kuondosha Funza wote chooni, ondosha kinyesi chote Funza wataisha automatically.

It needs very small mathematics, pambana na Ufisadi na Rushwa, hivyo ndiyo VICHAKA vya Mihadarati na uchafu mwingine. Ukishinda vita dhidi ya Ufisadi na Rushwa, mihadarati itajileta yenyewe central.

HUU MCHEZO HAUHITAJI HASIRA
 
Mi hii vita naichukulia ni vita ya big fishes against small finishes, Subiri tutaipima kwa mafanikio yake, yaani kuisha kwa mateja mitaani
 
Back
Top Bottom