The story of my interview failures and lessons learnt

hamna kitu kiliniuma kama ile siku niliyokuja hapo ofisini kwako nikiwa nina hustle at least nipate u volunteer, pale reception nilipo omba kuonana na HR wakanikatalia nikawaambia shida yangu walichofanya wakanipa form ya kujaza kama volunteer fomu yenyewe ni sawa na mtu anaeandaa disertation! nikajisemeza poa nikaideku nikasema ok..
nikaenda home mambo yakiwa bado magumu nikaona ni rudi tena duh hio siku ndo sito sahau maana nilikuwa na bahasha yangu ya CV nikapitiliza tena ili nikakutane na HR mara pap nikaambiwa kwa maombi ya kazi au chochote natikiwa ni ache CV pale getinkwa mlinzi nakumbuka nilirudi kama ili nishuke gorofa yenu niende nikampe yule mlinzi huku niendelea kuwa nikasema shuba miti yaani nimetoka huko uyole mpaka pale halafu nirudi bila ku mdekeree HR wai nikavuta handbrake nikapiga u-turn nikavizia PS kajipindua nikazama ndichi kwa HR wenu kule nako sijui nilikutana na na vivolunteer kashkaji kamoja kalinitolea mbovu ‘kwa sasa hatuajiri ‘ mie nikamjibu sitaki ajira ila nataka kujitolea’ wakati najibizana naye kwa upole na sauti yangu ya kutokea kooni nikauliza naomba kuongea na HR duh mara akaingia dada flani white anajisitiri basi moyo wangu ukawapasuka kwa furaha .. akaulizia nina shida gani ... nikamueleza akanisikia ila nikaongeza kuwa nataka kazi hata kama ni bure... akaniuliza fani yangu.. nikamjibu na nikaanza kushuka nondo za mradi wao mpango kazi wangu , matokeo yaani nilishuka kama vile niko CNN au kule wanapohojiwa mastaa.. kiukweli yule dada alifurahi akaipokea bahasha yangu kwa ajili ya reference na akaniambia baada ya wiki watatoa tangazo la kazi hivyo niombe na watatoa kupia gazeti au ule mtandao..
basi ndo hivyo walivyonitoa, nikasubiri hio wiki duh hola, mara hola holaaa kimyaa. duh nikawa najilaumu kwanini sikuchukua ile namba ya yule HR.

kwa hio kama ulivyoteseka brother kuipata hio position basi hao majamaa wanaojitolea hapo jaribu kuwa fevour na kuwasaidia kwa namna yeyote pia sio vizuri kuwaambia wateja wenu wanaotaka kazi wakaziache kule kwa mlinzi kiukweli inatia hasira maana kwa mlizi penyewe ni pale nje na huko palivyo na upepo na mvua mara mabahasha yetu kuyaacha exposed vile sio vizuri.

kwa sasa nipo kitaa naangalia ndinga zenu zinavyokatiza vijijini huku wakikusanya viazi na ndizi baada ya kutoka kwenye miradi yenu.
 
Duuhh!!
Hao wote uliowa describe nawafahamu.
Sina cha kusema zaidi ya kukwambia kwamba usichoke kupambana. Ipo siku utafanikisha malengo yako.
Mungu akubariki sana kijana katika mihangaiko yako na matamanio yako!!
itara
 
Uzi huu umeponya wengi, God bless you brother
 

Daaah pole sana
Mm nimewahi uzuria interview zao
Kuna changamoto nyingi sana pale ndani
Kupeana nafasi pia ni kwingi
 
Nimejikuta nikiisoma tena hii comment yako wakati huu... nimeshahama from this organization, pia hao jamaa wa HR wote ambao umewataja hapa walishapigwa redundancy wote.
Dunia ni duara.
itara
 
Nakubaliana nawe asilimia mia moja, kwangu ilitokea hivi baada ya kusota about two years nikaamua kujitolea kufanya kazi bila malipo na taasisi fulani ambayo baadae walianza kunilipa posho kutoka na bidii na nidhamu niliyokuwa nayo.

Then nikaona tangazo la ajira kwenye net Ila Kenya nika apply baada ya wiki nikaitwa through email pale Haile Silassie avenue Agip house opposite na Central Bank tulikuwa watu kama sita hivi nikajipima nikaona duh hapa sijui kama ntatoboa maana jamaa wanashusha ngeli ya Scotland hii yangu ya St Kayumba itapita kweli.... But during the interview I felt the panel was delighted with my answers, I was confident and calm. Mungu ni mwema nikaipata hiyo kazi, niliifanya vyema for two years and eight months then nika resign baada bi mkubwa wangu kupata maradhi yaliyohitaji niwe karibu nae.

Nikarudi bongo nikakomaa ilinichukua tena a year kuamua kutafuta kazi baada ya bi mkubwa kupona. Next position nayo nili appy kwenye net tu nikaitwa nikapiga vizuri kiasi maana was an international organization panel nzima whites na HR manager ndo mbogo hakuna anaenijua wala nae mjua. Mungu Ni mwema pia nikatoboa nilipiga nao mpaka nilipo amua kuacha mwenye nifanye kazi binafsi.

Vijana wasiogope, wasikate tamaa wala kutegemea godfather's sana jiamini omba kila nafasi ya carrier yako Mungu akuachi ukimtanguliza, pia ukiweza kuanzisha ajira yako bila kuajiriwa ni jambo zuri zaidi Kama una self discipline, leadership na uko creative and innovative.
 
Mkuu huu uzi unastahili heshima sana.

Kwa ufupi interviews nilizofeli mpaka sasa.
Stanbic
Standard Chattered Bank
BRELA
TAA (Mara mbili)
Nyati Cement
Metro
NMB
DTB

Ila sikomi na bado nakomaa though mpaka leo bado sina ajira
 
Mkuu nimekusoma vizuri kila baada ya nukta ...naomba kufahamu kwanini sehemu uliyopatia kazi uliendelea kukomalia zaidi tofauti na sehemu za mara ya kwanza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…