The story of my interview failures and lessons learnt

Miaka kadhaa iliyopita nilimalimaliza digrii yangu uhandisi kutoka chuo kimoja kipichopo hapa Tz. Mwaka ukakatika niko tu home sina hata jero mfukon alafu nikiangalia vyeti vyangu basi napata hasira kweli!!

Nikawa najiuliza ni wapi nimekosea kwenye maisha? Ikaja interview ya kwanza nikaigwa chini, ya pili nikapigwa chini basi nikawa mpole nikaridi home kuugulia maumivu!!

Mwaka jana ajira utumishi zikatoka, daah nikawaza nirudi hadi chuo kuchukua cheti wakati sina hata buku mfukon....nikataka kupotezea, nikawaambia madogo majibu waliyonipa nikaumia kweli kweli... Hawakunielewa nilipowaambia nataka potezea ile post!!

Mpango ukafanyika nikapata nauli... Huyo mpaka chuo kichukua cheti!! Nikaaply...

Baada ya jina langu kutokea nikaanza kupiga msuli kama niko chuo... Nilipitia kila notes kila kitabu... Google na youtube vilikua rafiki yangu[emoji23]

Mungu si athman nikaitwa kwenye oral, daah swali likaja tena nauli ya kwenda dsm napataje? Anyways nikafanikiwa kupata... Safari ikaanza mpaka utumishi dsm!

Zamu yangu ikafika nikaitwa, nikapigwa maswali mengine napata mengine nakosea ila nilikua siachi kutoa jibu bila kujali la kwelj au la!!

Mwisho alikua anaongoza interview akaniambia "i like your comfidence" nikajua anazingua baada ya kukosea maswali!!

Nikatoka zangu huyo mpaka gesti nikajiandaa na safari ya kurudi home kesho yake...

Mwezi ukapita majib yakatoka, Mungu mkubwa jina langu nikaliona... Nilifurahi sana... Kama sio madogo kunipa moyo nisinge apply!!

Baada ya stress za kitaa sasa niko kazin kama mhandisi...

Nilichojifunza...

Kwenye interview yeyote JIANDAE vya kutosha pili wakati wa interview JIAMINI hata kama hujui jaribu kujibu...
 
Inspiring [emoji120]
 
asante mkuu
 
Hii thread imenipa nguvu na kuamini ipo siku nitafanikiwa ni kuendelea na mapambano na kujisahihisha !! Nimefanya interview mbili zote Tanesco na zote nimefanikiwa kuingia kwenye oral na nikiwa kwenye top 2 kwenye written lakn zote sikufanikiwa kupata kazi !!
 
Kwani Tanesco Written wanatoa na Marks mkuu?
Vipi umeomba hizi zilizopitia PSRS?
 
Inspiring and very motivational, wacha tuendelee na kupambana. Wakuu kama kuna yoyote alifanya interview za TCRA zilizotangazwa December mwaka Jana anipe mrejesho, wanatumia muda gani hadi kuita watu kwenye interview maana naona kupokea maombi tu inachukua mwezi mzima.
 
Nimepata funzo kubwa sana kupitia kwako mkuu, ahsante nami nimejifunza kwakweli.....

I will never give up...[emoji1320]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…