The State of the Union address | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The State of the Union address

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WildCard, Jan 26, 2011.

 1. W

  WildCard JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Na sisi kama Watanzania tunao Muungano wetu. Rais wetu wa JMT naye angekuwa na hotuba yake kila mwanzoni mwa mwaka akalihutubia BUNGE pamoja na BARAZA LA WAWAKILISHI kwenye kikao cha pamoja akaongelea kwa undani mambo ya Muungano na kero zilizopo kama ifutavyo:
  -Mambo ya Ndani
  -Utendaji wa vyombo vyetu vya dola kama Polisi, Uhamiaji, Magereza.
  -Usalama wa ndani wa raia na mali zao.
  -Masuala ya Uraia, vitambulisho.
  -Mambo ya nje na ushirikiano kimataifa
  -Sera yetu ya Mambo ya Nje.
  - Utendaji wa Mabalozi wetu huko Ughaibuni.
  - Mabalozi wa Nje walioko hapa Nchini.
  - Wawekezaji wa Nje hapa nchini.
  -Jumuia mbalimbali za kiuchumi ambazo sisi ni Wanachama:
  EAC, SADC,etc.
  -Jumuia za kisiasa na kijamii ambazo sisi Tanzania ni Wanachama:
  UN, AU,ICC,....
  _Masuala ya fedha na mgawano wa madeni, mikopo,ruzuku,misaada.
  -Masuala ya ajira, mawasiliano, miundombinu,...
  -Mambo ya KATIBA ya JMT.
  -Masuala ya DINI na UMOJA wa KITAIFA.
  Yapo pia mambo mengine mengi ambayo Rais wa JMT na wasaidizi watakuwa wanaona ni muhimu kuwashirikisha Watanzania kwa ujumla wao. Umefika wakati sasa tuvipe umuhimu vikao vya KISERIKALI nguvu zaidi hata kuliko vile vya VYAMA vyetu. Vikao hivi vya kiserikali ni vyetu wote kama Watanzania tofauti na vile vya VYAMA ambavyo ni kwa ajili ya wanachama husika na vina matabaka, ubaguzi na usiri mwingi mno.
  Naomba kuwasilisha.
   
Loading...