The South African Truth and Reconciliation Commission (TRC)

chasusa27

New Member
Feb 24, 2008
3
45
Wana Bodi, Salaam.

Je, Watanzania hatuhitaji tume ya ukweli na upatanisho kama ile ya South Africa kushughulikia masuala ya uvunjanji wa haki za kibinadamu kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi hayati Magufuli?

Maneno mengi yanasemwa na kwa mawazo yangu kuna pande mbili katika hili jambo.

Wale wanojiita wanyonge na kuttetewa na huyu mshemiwa mwendazake na wale walioumizwa na kuvunjiwa haki zao za msingi kama raia .

Tulishuhudia nyumba zikivunjwa maeno ya Kimara Dar es salaam bila fidia yoyote.

Kule Mwanza zoezi hilo halikufanyika chini ya utetezi wake kwamba wale ni wapiga kura wake.

Baadhi ya wananchi pesa zao benki zilizuiliwa bila kupewa sababu za msingi na bila kufuta sheria husika.

Wakuu wa Mikoa na Wilaya walikuwa na nguvu kubwa kuwa adhibu wananchi na kuwaweka kifungoni kwa sababu binafsi.

Mashamba yalinyang'anywa na huharibifu mkubwa kufanyika. hawa wote walikuwa hawana pakusemea kutoka na nguvu kubwa za dola kutumika.

Je, haujafika wakati muaffaka wakapata jukwaa la kupeleka malalamiko yao na kusikilizwa?

Kumezuka mtindo wa kutoa press conference kuzungumzia maumivu yao lakini wanakabiliwa na shutuma kutoka upande wapli kuwa hawaheshimu Marehemu kwani hata pata jukwaa la kujitetea.

Kwa midhali hii basi naomba Serikali ikaunda tume kama ile ya SA tujue mbivu na mbichi zipi ili jambo hili lishughulikiwe na tuachee kujenga chuki na umbea ili Nchi yyetu isonge mbele na mtizamo mpya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom