The samianism of mineral extraction in wildlife protected areas: je tunalionaje?

Conservator

Member
Jun 26, 2017
79
110
Helo WanaJF,

Jana tarehe 06/04/2021 alipokuwa akiwaapisha Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu na Wakuu wa Taasisi za Serikali, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo ya kuangaliwa upya uwezekano wa kuchimba madini yaliyopo kwenye maeneonya hifadhi hasa hifadhi za wanyapori zikiwemo zilizopo chini ya TANAPA (Mbuga za Taifa).

Katika hotuba yake, alieleza kuwa kwa muda mrefu baadhi ya viongozi akiwemo Kamishina Mkuu wa TANAA na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dr. Allan Kijazi wamekuwa wakikataa kuruhusu uchimbaji wa madini ndani ya hifadhi kwa sababu za kimazingira na kiikolojia.

Mhe. Rais pia alielezea kuhusu gesi ya helium ambayo inapatikana katika Bonde la Mto Rukwa ambayo pamoja na gesi hiyo kuwa na tija kubwa kwa taifa, muwekezaji amekuwa akizingushwa mpaka sasa. Soma saidi kuhusu ugunduzi wa helium hapa.... Gesi ya Helium Yenye Uwezo wa Kukidhi Mahitaji ya Dunia Nzima kwa Miaka 20, Kuanza Kuchimbwa Tanzania mwakani

Mhe. Rais alieleza kuwa ni vyema kupima "opportunity cost" ya kuchimba madini katika hifadhi. Anaamini gharama ya kuacha kuchimba yaweza kuwa kubwa ndogo ya kutochimba. Kwa maana nyingi ni sawa na kupima kati ya manufaa na hasara ya mradi wa aina hiyo.

Alieleza kuwa kuacha madini kwenye hifadhi hakuna tija kwa sababu madini hayo sio kwamba ni yanaliwa na wanyama na kwamba kuyachimba hakupunguzi share ya chakula cha wanyama.

Alieleza kuwa kama ikibidi, ni bora hata kugawa eneo la hifadhi ili eneo moja libaki kama hifadhi na lingine libaki kama eneo ya kuchimba madini.


MY TAKE
Nimetumia neno au msamiati "SAMIANISM" kujaribu kuunganisha mtizamo wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika neno moja.

SAMIANISM laweza kumaanishi mtizamo wa Mhe. Rais kiuchumi, kisiasa, kijamii, kimataifa na hata kimazingira.

Katika mada husika, SAMIANISM haijalenga Madini tu bali maliasili kwa ujumla. Na sio maliasili zilizopo katika maeneo lindwa ya wanyapori tu kama hifadhi za taifa na mapori ya akiba, bali kwenye maeneo yote lindwa ya kimazingira yakiwemo vyanzo vya maji, hifadhi za misitu, maeneo oevu na maeneo ya bahari.

Suala la uchimbaji wa madini kwenye hifadhi najua linafanana sana na masuala yaliyojadiliwa zaidi yakiwemo mradi wa Kufua Umeme katika bwawa la Nyerere lililopo ndani ya hifadhi ya Selous, kupitisha barabara kuu katikati ya Mbuga za wanyama hasa Mikumi na Serengeti pamoja na masuala mengine.

Kimsingi siku zote when comes to Economic Intrests Vs Conservational Interests kumekuwa na mjadala mkali.

Kwa mtizamo wangu, mambo maamuzi kama haya nafikiri ni vyema yakaamuliwa kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu hasa kupitia Impacts Assessments and Cost-Benefit Analysis

KWENYE UCHUMI, the future is uncertain and you never know future generation might be brighter than us. And so far, tunafanya maamuzi haya ili tupate fedha za kujenga miundombinu ya barabara, afya, elimu na mengine ambayo pia itakuwa na faida kwao. Ni kama tunawakopa kwa ajili ya manufaa yetu na wao.

Halafu so far, what is resource? Nani alikua anajua kuwa Coal itakuja least preferable resource when comes to fuel? Kwa hiyo resource inategemea na uelewa wa watu kwa mda husika. Si ajabu uko mbeleni watu wakagundua kuwa ukichanganya resource fulani na resource nyingine unapata gesi bora zaidi kuliko helium. Kwa hivyo wala tusiwe na wasi kuhusu what is called future generation au sustainable development. Kwanza iyo kesho nani ana uhakika kuwa atakuwepo 50-100 ijayo?

Na mwisho kabisa, kwani Wanyama au miti si tunaweza kuvizalisha tena? (Renewables). Why worrying for something that can be regenerated?

COST-BENEFIT ANALYSIS yaweza kuwa ndio kipimo kikuu cha kufanya maamuzi katika maslahi yankiuchumi.

KWENYE UHIFADHI

Kila kiumbe hai au kisicho hai (both biotic and abiotic) kina umuhimu katika ikolojia. Kabla ya kufanya maamuzi ni vyema tukajiridha juu ya uendelevu wa ikolojia iliyopo. Unapochimba madini kwenye hifadhi, utaharibu mazingira, utakimbiza wanyama, utaharibu mfumo wote wanikolojia na mazingira asili. Maamuzi ya sasa yanaweza kuwa na tija kiuchumi kwa sasa lakini manufaa hayo hayatadumu (sustainability) na kwa sababu madini yakiisha yameisha. Vizazi vijavyo vitaishi kwa shida.

Mwl. Nyerere angetaka angetumia sana rasilimali madini lakini aliacha kwa vizazi vijavyo kama sisi, hivyo na sisi tuna jukumu la kutumia vizuri ili na vizazi vijavyo na nyenyewe vifaidike.

Ni vyema kufanya maamuzi hayo kwa kutumia ushauri wa wataalamu uliotokana na Tathamini za Athari za Kimazingia na Kijamii (EIA na SIA) au Tathamini za Kimkakati za Kimazingira (Strategic Environmental Assessment) ambazo zipo kwa mujibu wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 sheria zingine za kisekta kama sheria ya misitu, wanyapori na ardhi.

Pamoja na mambo mengine, EIA, SIA au SEA zinasaidi kutambua kwa namna gani mradi unaopendekezwa unaweza kuathiri ikolojia ya eneo husika, viumbe waliopo, jamii inayozunguka pamoja na kushauri namna gani ya kupunguza (mitigation) athari hizo kama ukiruhusiwa au kushauri mradi usitekelezwe kabisa.

Nimejaribu kuzungumzia pande mbili, Naamini wataalamu wa mazingira na uchumi wataeleezea zaidi.


Mwisho nitumie fursa hii niseme kuwa JamiiForums imetunyima Jukwaa la Mazingira na pamoja na maombi lakini bado suala hilihalijatekelezwa.

Naungana na wadau wengi kuiomba JF ituwnzishie Jukwaa Mahsusi kwa ajili ya kujadili masuala yote yanayohusiana na uhifadhi, utunzaji na usimamizi wa Mazingira pamoja maliasili kwa ujumla.

Niliwahi kuanzisha uzi huu:

Utunzaji na Uhifadhi Endelevu wa Mazingira na Maliasili Tanzania

Karibuni.!
 
Huko hakuna faida inayopatikana,hivi sijawahi kusikia mbuga za wanyama zimeliingizia Taifa kiasi gani cha dolari, tuna mbuga nyingi kuliko ulimwengu wowote ule japo tupo ulimwengu wa pili hizi mbuga ni mzigo,watu wagawane nyama yaishe waTanzania tunzazaliana kwa kasi na tunahitaji eneo,mbona kuna nchi zinayo zoo tu na zinaingiza hela kuliko hapa msituni.

Mabeberu kama wanataka wanyama waje kuchukuwa sisi tumeshawachoka,simba wanatuvizia ,tembo huingia mashambani ni balaa tu,
nashauri yafanywe mabadiliko wale wananchi wangororo wahamishwe na wale wanyama wa kule kunakotakiwa kuchimbwa madini wabadilishane.Ikizingatiwa kupeleka huduma za jamii ndani ya ngorongor ni shida,
 
Huko hakuna faida inayopatikana,hivi sijawahi kusikia mbuga za wanyama zimeliingizia Taifa kiasi gani cha dolari, tuna mbuga nyingi kuliko ulimwengu wowote ule japo tupo ulimwengu wa pili hizi mbuga ni mzigo,watu wagawane nyama yaishe waTanzania tunzazaliana kwa kasi na tunahitaji eneo,mbona kuna nchi zinayo zoo tu na zinaingiza hela kuliko hapa msituni.

Mabeberu kama wanataka wanyama waje kuchukuwa sisi tumeshawachoka,simba wanatuvizia ,tembo huingia mashambani ni balaa tu,
nashauri yafanywe mabadiliko wale wananchi wangororo wahamishwe na wale wanyama wa kule kunakotakiwa kuchimbwa madini wabadilishane.Ikizingatiwa kupeleka huduma za jamii ndani ya ngorongor ni shida,

Asante Mkuu.

Wacha tusubiri wengine wanasemaje
 
Back
Top Bottom