The rise and fall of young Africans Sc

Ladder 49

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
7,416
18,856
Wakuu habari zenu?

Kuanzia msimu wa 2017 mpaka sasa young africans sc mwenendo wake umekuwa sio mzuri timu inazidi kupoteza uwezo wa kiushindani kwenye ligi na msimu unakuja itazidi kushuka kama ilivyopoteza uwezo msimu huu,maana wamekuwa na kelele nyingi ambazo aziwapi matokeo.fukuza fukuza nyinyi na timu kutokuwa na malengo ya muda mrefu.

Kwa wale wanaofatilia ligi ya vpl msimu huu wa 2019/2020. Kwa hali ilivyo kwa timu ya young africans sc.

Msimu huu hii timu imeshuka kiwango maneno yamekuwa mengi kushinda vitendo vya uwanjani.
Inaonekana wachezaji hawafundishwi mpira kama vile forwards hazifundishwi kulenga goli sasa kama ndio hivyo kwenye mazoezi wanafanyaga nini au wanakimbia tu na kupeleka mpira mbele.

Kwa hali ilivyo kwenye msimamo wa ligi inashika nafasi ya tatu tofauti ya point mbili na timu ya juu yake na timu ya chini yake na mechi zimebakia 9 Baada ya kucheza mechi 30.

Kuna uwezekano mkubwa young africans sc ikamaliza ligi ikiwa nafasi ya 4 ,mchezaji mwenye magoli mengi kwenye timu ya young africans sc ni molinga(falcao) ana magoli 8 Baada ya mechi 30 kuchezwa.


Kwa hali ya uwezo wa kucheza uwanjani kwa sasa young africans sc inakwenda kupotea kwenye kimataifa,hizo timu ambazo wanashindania nafasi ya pili hawana migogoro yoyote kwenye timu yaani zimetulia ila young africans sc timu aiko vizuri kelele nyingi ambazo azisaidii timu kupata ushindi.

Msimu huu ni tofauti na msimu mingine ya huko nyuma wanaposhindana simba sc na young africans sc timu zinazofata nyuma zinakuwa zimeachwa nyuma point nyingi sana.lakini msimu huu wa 2019/2020 umekuwa tofauti sana.


Young africans sc msimu huu wamesajiri lakini mchezaji mwenye magoli mengi anamagoli 8 kwenye mechi 30. Kingine ni kwamba hawana hela za kusajiri ili kuzibomoa timu ndogo zilizojuu msimu huu kama namungo, azam na jkt Tanzania,coastal union kwa hiyo ataendelea kupewa ushindani kupata nafasi ya pili.

Usimu ujao wataanza kuwa wa matopeni kama walivyokuwa wanawaita wenzao.mpira ni mchezo wa hadharani kila mtu anaona hakuna janja janja kwa sasa.


Kwa jinsi msimamo ulivyo na hali aliyokuwa nayo hawana uwezo wa kumaliza nafasi 3 za juu mechi zimebakia 9 na mechi ya kesho anacheza na namungo ambae amemzidi point 2, namungo hawana chakupoteza, namungo wako vizuri sana.young africans sc angekuwa na uwezo au kweli kama anaitaka nafasi ya pili angeshinda mechi na azam angeonesha kweli anania.

mechi na azam imetoa picha kamili kwa uwezo wa young africans sc msimu kama kweli walikuwa wanataka kuchukua nafasi ya pili wangemfunga azam,lakini kwa wale tulioangalia mpira bila kupepesa macho hawana huwezo wa kuchukua nafasi ya pili.

Msimamo wa ligi huo hapo chini.

IMG_8291.jpg




Ni hayo tu wakuu.
 
Kawaulize washamba wa awamu ya tano kwa nini Yanga legelege usijifanye unaishi Cambodia 🇰🇭
 
Yanga ni timu nzuri ila ishu kubwa ya Yanga ipo kwenye uongozi tu,kama viongozi wanaelewana na wachezaji pia wanaelewana hata timu iwe na wachezaji wabovu lazima kuna spirit ,Yanga inakosa spirit tu
 
Viongozi wa YANGA ACHENI UTAPELI.
mnasema Morrison kasaini miaka 2.
Wakati mkataba wake unaisha MWEZI UJAO?.
Tena mlimpa miezi 6.
Ujanja ujanja utawapeleka wapi?
Screenshot_20200624-083907.jpg
 
Back
Top Bottom