The Real Hidden World


Unaweza kututhibitishia kwamba hayo uliyoaona au kuyajua kuhusu ulimwengu wa uliofichuka ni ya kweli?
 

Kaka naona mambo madogo sana umeyapa hadhi isiyo stahili.

Mada nzima ni Uchawi,na kitu ulichokosea ni kutokujua asili ya hiyo elimu uliyoisoma humo na kujua ni elimu gani.

Hili swali nakuachia au naweza kukupa ziada,babu yako achilia mbali alikichoma kitabu hicho,lakini ukweli Uchawi huwa unateketezwa kwa moto yaani kuchomwa.

Elimu ya nyota yaani unajimu,kiistilahi ya kielimu ni Falaki/Falaqi hizi ni elimu za kishirikina zenye kupata msaada wa karibu wa shetani na si vinginevyo. Hukumu ya elimu hii haipaswi mtu yeyote kujifunza kwani ni mtihani kwa mwanadamu na madhara yake ni makubwa sana hasa kwako mwenyewe mfanyaji au mwenye kujifunza elimu hiyo.

Umezungumzia suala la yule nduguyo aliyefatwa na jirani na kuulizwa kuhusu hatima ya wawili,jambo liko wazi hata bila ya kuwa na kitabu hicho,na kuna yale unayotakiwa kuyanya wagonjwa wakiwa katika hali hizo.

Lakini,je unaweza kutuhakikishia ya kuwa je ni kwa kiasi gani tusimtuhumu ndugu yako juu ya kuhusika na vifa vya hao ndugu wawili,kwa yeye kujihusisha na elimu ya uchawi ?

Hitimisho juu ya kitabu hicho.

Je unaweza kuniambia muandishi wa kitabu hicho na mwaka alio kiandika kitabu hicho yaani kutoka kwa mara ya kwanza na kuanza kutumika ?

Nipo ....
 


Umenena vyema mkuu ni uchawi totaly sikupingi ulichokiongea,
Ila naomba nikurudishe tena urudie kusoma, utakaposoma mara hii jaribu kuzingatia pande mbili zote nilizozieleza,
Jaribu kuangalia upande wapili niliouandika japo haujauzingatia soma kama haujui kitu utaelewa nini namaanisha, ukisha maliza kusoma rejesha maarifa yako tena.

Pia mkuu jifunze Kwa mfano huu
Sio wote wanaofanya kazi katika kiwanda cha bia ni walevi,
Sio wote wanaolima tumbaku basi huvuta sigara,
Sio kila wanaosoma hukichukua kile walichosoma,

Kwahiyo unapojaribu kuzungumzia baadhi ya hoja zingatia ya kujua kazi za matamshi yaliyotumika katika uandishi ili kujiepusha kumpa mtu uhusika ambao hana,
Unauelewa mzuri ila huwa unaharakisha kuelewa jambo badala ya kutulia na kutafakari,
Hizi post wamesoma wengi sana lakini wengine wameacha kama yalivyo na wala hajawasumbua.

Pia ukiangalia hicho kitabu unachohitaji kujua mwandishi na mwaka kiliotolewa iko hivi,
Sio kila kitabu huwekwa kwa ajili ya kuuzwa na kusomwa na kila mtu,
labda nikupe ukweli kidogo kuhusu hicho kitabu
Ukigoogle namna ya kukisoma mtandaoni huwezio kupata ukweli hata siku moja, wala hautakuja kupata mtu mwenye maelezo sahihi namna ya kusoma,
Watu wamekuja inbox wanataka kujifunza kujua kukisoma nimewapa athari zake kwanza na nimewaambia mimi sijawahi kujaribu kusoma hata siku moja wala sihitaji nikisome.

Pia kilipoandikwa ilikuwa ni kama diary ambayo ilitumika kwa miaka mingi sana kabla hawajaanza kufanya copy so usiwe unakariri mkuu jaribu kuwa mtu wa hoja za kujifunza sio za ujuaji
 
Unaweza kututhibitishia kwamba hayo uliyoaona au kuyajua kuhusu ulimwengu wa uliofichuka ni ya kweli ?
Laiti kama ungelielewa hoja nilizoziandika basi usingeliuliza swali kama hili
 
Pia mkuu jifunze Kwa mfano huu
Sio wote wanaofanya kazi katika kiwanda cha bia ni walevi,
Sio wote wanaolima tumbaku basi huvuta sigara,
Sio kila wanaosoma hukichukua kile walichosoma,

Huu mfano hapa umeubabatiza,mim siongelei hali hiyo,bali mimi nina ongelea kufanya. Hapa nakujuza sio kila elimu unapaswa kujifunza,kwani kuna elimu kujifunza kwake tu ni makosa na kuifanyia kazi ni kosa zaidi.

Mizani ya ukweli wa mambo iko hivi,tukianza kumtafuta mbaya tuna anzia nani wa kwanza katika kusababisha kisha tunakuja kwenye matokeo. Mizani ya haki hata watengeneza pombe na wassinywe wanaingia katika makosa ya kushiriki katika kudhoofisha afya ya akili ya wale wakusudiwa katika pombe hiyo,na mfano huu unaingia katika tumbaku vile vile. Huu sasa ndio ule upande wa pili wa elimu iliyosahaulika.

Bado mfano wako haujakidhi haja ya kudhoofisha hoja yangu.

Naendelea ....
 

Hapa nakupa akiba ya hili swali. Ushawahi kujifunza historia ya UCHAWI ?

Narudi kuendelea kujibu hoja yako ......
 
Hapa nakupa akiba ya hili swali. Ushawahi kujifunza historia ya UCHAWI ?

Narudi kuendelea kujibu hoja yako ......
Sio kujifunza nimesoma historia ya uchawi na makala mbalimbali za uchawi na hata vitabu mbalimbali
 
Kujifunza sio kosa kosa ni kutenda jambo lililokinyume na misingi ya taratibu zinazotuzunguka
 
Kujifunza sio kosa kosa ni kutenda jambo lililokinyume na misingi ya taratibu zinazotuzunguka

Hapa ndipo tunapotofautiana mimi na wewe,na huu unaweza kuwa mjadala pweke au mada yenye kujitegemea.

Unaweza kuniambia au kunipa faida ya kujifunza UCHAWI ?

Ni ipi mizani yako juu ya kujifunza jambo au elimu ? Yaani kwako wewe ili jambo uweze kujifunza lazima liwe na sifa gani ? Ni upi uhhsiano kati ya faida,madhara na kujifunza elimu husika ?

Kwa mfano mimi kwangu mimi ni makosa kujifunza Uchawi,Falsafa,Elimu ya Nyota(Falaki),Muziki,Mantiki (Logic),je unaweza kunipa hoja za ulazima wa kujifunza elimu hizo nilizo zitaja ?
 

Unaweza kuniambia au kunipa faida ya kujifunza UCHAWI ?


MKUU UNAUELEWA MKUBWA ILA SIJUI UNAFELI WAPI NIKUPE FAIDA ZA KUJIFUNZA UCHAWI KWANI MIMI NI MCHAWI?
AU UMESIKIA MIMI NAFUNDISHA UCHAWI?
TAFUTA MWALIMU WA UCHAWI KISHA MUULIZE MASWALI HAYO

NA NIMEKUAMBIA SIJAJIFUNZA UCHAWI ILA NIMESOMA MAKALA MBALIMBALI ZA UCHAWI HEBU TOFAUTISHA BASI MWANAFUNZI NA MSOMAJI


HAYA SWALI LAKO LA PILI
Ni ipi mizani yako juu ya kujifunza jambo au elimu ? Yaani kwako wewe ili jambo uweze kujifunza lazima liwe na sifa gani ? Ni upi uhhsiano kati ya faida,madhara na kujifunza elimu husika ?

MIZANI YANGU YA KUJIFUNZA JAMBO HUANZIA KATIKA SWALI KWANINI? BAADA YA HAPO NAANZA KUTAFUTA MAJIBU NINAPOANZA KUTAFUTA MAJIBU TAYARI NAKUWA NIMEJUA HILI JAMBO LAFAA KWA MAARIFA KWANGU NDIO MAANA NAENDELEA KULITAFUTIA MAJIBU.
PIA ILI JAMBO NIWEZE KUJIFUNZA NI LAZIMA LIWE LIPO KATIKA NJIA YA MISINGI NINAYOITUMIA (UNAWEZA USIELEWE SABABU NI KITU BINAFSI)
UHUSIANO WA FAIDA NA HASARA NI KWAMBA HUWA NAGUNDUA NAPATA HASARA NILIPOKUWA SILIJUI LILE JAMBO, NDIO NATAFUTA MAJIBU YAKE ILI NIANZE KUPATA FAIDA ZAKE


HAYA SWALI LAKO LA TATU
Kwa mfano mimi kwangu mimi ni makosa kujifunza Uchawi,Falsafa,Elimu ya Nyota(Falaki),Muziki,Mantiki (Logic),je unaweza kunipa hoja za ulazima wa kujifunza elimu hizo nilizo zitaja ?

SIWEZI NIKAKUAMBIA NI MAKOSA AU SIO MAKOSA KWASABABU NI JAMBO LAKO BINAFSI ILA NAWEZA KUSEMA KABLA HAUJAJIFUNZA JARIBU KUELEWA KWANZA KWA UNDANI NI NINI UNAHITAJI UJIFUNZE
KWAHIYO ULAZIMA WA KUJIFUNZA UNATOKANA NA SHAUKU YAKO BINAFSI WALA SIO MTAZAMO WANGU.

NB:ITIKA WITO KATAA NENO
 

Hapa nakujibu kwa kauli fupi sana,hujawahi kusikia mtu akisema, "Nimesoma kitabu hiki nimejifunza mambo mengi sana"

Niliona tangu mwanzo kwamba tamko "Kujifunza" unalieelwa kwa uchache sana,yaani lina kutatiza,hulipi haki yake.

Naimani hapa umenielewa.
 
Nakurudishia kauli fupi Sana
Sio kila tunachosoma tunajifunza
 
Jana niliipitia sana hii thread na nikajikuta na kuwa interested to know more. Baadae nikaingia chimbo kutafuta kitabu cha “Napoleon book of fate” luckily nikakipata. Baada ya kukisoma kidogo nikajua namna ya kufanya nacho kazi na nikajianzia mimi mwenyewe ili nione namna kinavyofanya kazi. Majibu niliyoyapata yanebifanya niamini kwa zaidi ya 80%. Sasa tatizo sitakiwi kuuliza swali linalonihusu mwenyewe zaidi ya moja kwa siku.

Anayehisi anataka kujua issue yako anaweza kuniuliza nikamuangalizia ili kuthibitisha nilichothibitisha mimi.

Naendelea kutaka kujua zaidi kuhusu ulimwengu uliojificha


Sent using JamiiForums For iPhone App
 
Nielekeze Mkuu how inakitumia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
No there is only one source of spiritual power and its GOD. But with two big qualities the Goods and Bads depending subject ommision action and object senses receiver buts all starts as equal and ends as one. Alpha and Omega.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefuatilia thread zako, wewe ni mdadisi na unataka kujua, tunafanana kasoro wewe ni mwoga na hutaki achia ulichokwisha kukiamini. Imani ni jambo la msingi sana, huwezi fanikisha safari yako kama huamini njia uichukuayo ni sahahi kwa asilimia zote. Lakini pia kunaathali kubwa ya kuamini utafika kama hujaanza tembea kuelekea unakopaswa kuelekea, ni sawa na waumini fulani waliokuwa pale Airport wakifanya maombie wakiamini maombi yatawapeleka Ulaya.

Binadamu hakuzaliwa hapa pasipo sababu, kuna sababu, jaribu kumchunguza mtoto mchanga anavyojaribu kukuza fahamu zake, kujiwezesha, kujifunza na jiulize ile effort imeishia wapi?

**** nitaendelea ****
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…