Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,253
- 44,591
- Thread starter
-
- #41
Nilitaka kuonyesha tu ni njisi gani sisi wote ni wezi tu na ndiyo maana nivigumu sana kukemeana. Ukianza tu kukemea roho inakusuta inakuambia kuwa hebu piga matumizi yako ya mwezi halafu toa kipato chako halafu nieleze hii difference umetoa wapi. Of course watu walio wengi wanapenda kuishi maisha ya haki na wanajikuta tu wameingia kwenye hii circle ya ufisadi kwa mazingira. Hebu fikiria fedha kiduchu halafu kuna hawa wenzetu wenye fedha basi utaona wanakopesha kwa Riba ukikopa laki mbili basi mwisho wa mwezi unaripa 240,000.
Kwa sasa ni mafisadi tu ndiyo wanaofaidi maana ukiwa na cash kidogo tu basi inaongezeka kwani raia ni choka mbaya
Mkuu, kuna watu Tanzania wanaoona hiyo kuwa ni bei poa tu. Kuna apartments zinajengwa Dar ambazo zinauzwa mara nne ya hiyo (ila sio one bedroom apartment, ni three bedroom apartments) na zinanunuliwa kwa kasi ya ajabu. Nyingine huwa zimeshauzwa kabla hata jengo halijakamilika.
There are people who are living while we are surviving.
Yes, we know, we are living in a corrupt society. What we need to articulate is the total failure of the government instrument which is responsible for fighting against corruption (PCCB), What this instrument is doing?? watching without doing nothing?? Indeed is watching that is why we are lamenting about the hardship Tanzanians are facing for the moment. Shame to PCCB
Shalom, mwishoni mwa mwaka jana niliandika makala moja ambayo nilisema kuwa wakazi wa Dar ndio wanufaika wakubwa wa ufisadi; nilichomaanisha ni kama hicho ulichosema; kwamba watu wa mjini wameweza na wanaweza kuishi katika mazingira ya kifisadi kwa sababu wao wenyewe vile vile wananufaika na ufisadi huo. Hii inafafanua ni kwanini upinzani hauwezi kushinda katika miji ya Tanzania kiurahisi, isipokuwa pale ambapo watu hawanufaiki sana na ufisadi huo.
Post imenigusa saana. Tuseme kwa ujumla wake wafanyakazi wanawaibia waajiri halafu wantegemea waendelee kuwa na kazi. Mh jamani sijui tunaelekea wapi. Mie nadhani suala la rushwa lianzie kwenye familia zetu. Wapo watu wanamalengo na wanahakikisha hawagusi rushwa na wanafanikiwa. Jamani hebu tuseme inatosha.Yes, sisi hasa wakazi wa Dar kama alivyosema mchangiaji mmoja ghafla ufisadi ukizimwa tutahangaika sana na wengi tutakufa njaa. Na pia kumbuka hawa mafisadi uchwara ndiyo wapambe wakubwa wa ccm
Kwa mfano jana nilimsindikiza mshikaji kununua LCD tv kariakoo bei inayouzwa ni Tshs 2, 200,000 kariakoo baada ya kubembeleza ikafika 1.9 chaa ajabu tukaambiwa bila kupewa risiti Tv inauzwa 1.5 na warrant ya miaka miwili unapewa, tukatizamana, tukatabasamu hapo hapo ufisadi ukafanyika. Ukipiga hesabu hapo VAT yetu ni 18% basi utagundua tu kuwa ile bei ya 1.9 ni ya kutisha watu ili wafanye ufisadi.
Ona hii kali kabisa ni ya haya mashirika yetu njisi yalivyo na wafanyakazi ambao ndiyo hatari kabisa. Maafisa wa TRA ndiyo hao wanatoka kazini na kwenda kwa wateja wao kuwafundisha jinsi ya kukwepa kodi. Ukitaka kutumia umeme kidogo kabisa kwa mwezi bila kupata bughza yoyote basi tumia wafanyakazi wa Tanesco kifix LUKU yako, watakuja na official seal na kukufanyia mambo ghafla ulikuwa unatumia umeme wa tshs 200,000 unashuka mpaka Tshs 5000 kwa mwezi. Inakuwaje jamani hawa watu wanakata mti walio kalia?
Sasa njoo hapa JF sema jamani tunataka tutokomeze rushwa weee! utaona njisi unavyotoka na matusi ya kila aina. Ni lazima kwa pamoja tuamue kujiosha na kubadili tabia na tutafanikiwa kwa kuanza na chama kipya raisi mpya na mambo mapya!
Mwanakijiji matumizi mabaya ya serikali watu hawaiti rushwa bali ni haki zao. Km unakumbukumbu nzuri utakumbuka jinsi akina Mwakyembe jasho lilivyokuwa linawatoka kujustify double allowance ni kitu cha kawaida kwa sababu ni utaratibu walioukuta. Wanasahau kwamba hata uchafu wa Richmond ni utaratibu walioukuta. In general rushwa hii watu wanaita haki yao.point well taken
this is part of corruption - corruption is not just bribery; it includes all these and more.
Sehemu chache zenye huduma zinazoridhisha (kama mijini) si zingekuwa na ushindani wa kibiashara na hivyo kupunguza bei? Kwanini sehemu hizo ndizo zina gharama kubwa zaidi?
Yes, sisi hasa wakazi wa Dar kama alivyosema mchangiaji mmoja ghafla ufisadi ukizimwa tutahangaika sana na wengi tutakufa njaa. Na pia kumbuka hawa mafisadi uchwara ndiyo wapambe wakubwa wa ccm
Kwa mfano jana nilimsindikiza mshikaji kununua LCD tv kariakoo bei inayouzwa ni Tshs 2, 200,000 kariakoo baada ya kubembeleza ikafika 1.9 chaa ajabu tukaambiwa bila kupewa risiti Tv inauzwa 1.5 na warrant ya miaka miwili unapewa, tukatizamana, tukatabasamu hapo hapo ufisadi ukafanyika. Ukipiga hesabu hapo VAT yetu ni 18% basi utagundua tu kuwa ile bei ya 1.9 ni ya kutisha watu ili wafanye ufisadi.
Ona hii kali kabisa ni ya haya mashirika yetu njisi yalivyo na wafanyakazi ambao ndiyo hatari kabisa. Maafisa wa TRA ndiyo hao wanatoka kazini na kwenda kwa wateja wao kuwafundisha njisi ya kukwepa kodi. Ukitaka kutumia umeme kidogo kabisa kwa mwezi bila kupata bughza yoyote basi tumia wafanyakazi wa Tanesco kifix LUKU yako, watakuja na official seal na kukufanyia mambo ghafla ulikuwa unatumia umeme wa tshs 200,000 unashuka mpaka Tshs 5000 kwa mwezi. Inakuwaje jamani hawa watu wanakata mti walio kalia?
Oh utakimbia bei za LCD/Plasma kwa Tanzania utashangaa kabisa. Tena basi nyingi ni fake. Yaani rushwa rushwa!!!Naomba niulize make ya hiyo LCD na size yake, if you don't mind.
mfano mzuri sana huo
Naomba niulize make ya hiyo LCD na size yake, if you don't mind.
Samsung, series 4 inch 42 model sikumbuki labda nikeenda kwa mshikaji nitapiga chabo. Price yake ukiangalia kama Amazon nadhani ni USD 700 kama sikosei
Kwa Tanzania hiyo inauzwaje?
Ni kitu gani kinafanya LCD hiyo kuuzwa karibu mara mbili ya gharama kwenye nchi hizi za kigeni? au watu wanataka kutengeneza faida asilimia 100 ya gharama ya uingizaji?