The Queens Gest yafungwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The Queens Gest yafungwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 28, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  UONGOZI wa Ofisi ya Kata ya Kigogo umeifunga rasmi nyumba ya kulala wageni inayotambulika kwa jina la The Queens iliyopo pembezoni mwa Shule ya Sekondari ya Kigogo ambayo ilikuwa ikilalamikiwa na wanafunzi wa shule hiyo
  Kufungwa kwa nyumba hiyo kumekuja baada aya gizo kutoka kwa Meya na makubaliano yaliyofanyika baina ya uongozi huo na mmiliki wa gesti hiyo.

  Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kigogo, Emmanuel Riwa alibainisha kuwa, katika mazungumzo hayo walikubaliana nyumba hiyo mmiliki huyo aibadilishe kutoka ya kulala wageni na iwe katika mfumo wa kawaida ya kupangisha watu kwa ajili ya makazi

  Alisema nyumba hiyo kwa muda uliobaki utapangisha kama makazi kusubiria shughuli ya tathimini na ulipaji wa fidia itakapokamilika kutoka Manispaa kwa ajili ya mazingira hayo kuwa ya shule.

  Hata hivyo pia wameadhimia kufunga gesti hiyo kutokana na kuona inachangia mmomonyoko wa maadili kwa wanafunzi wa sekondari hiyo .

  Wanafunzi washule hiyo walioongea na nifahamishe walionekana kufurahishwa na hatua iliyochukulia na Meya wa Kinondoni na kusema nyumba hiyo ingeweza kuwaporomosha kimasomo kutokana usomaji ulikuwa mgumu

  “Yaani tumefurahi ujue nyumba yenyewe ilikuwa ikitoza shilingi 1,500 kiwango cha chini, ingeweza kuharibu wanafunzi wanaopenda ngono za utotoni kwa kuwa wangekuwa na uwezo wa kulipia”walisema
   
 2. M

  Mutambukamalogo JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Comment ya huyo mwanafunzi haijakaa sawa. Swala la kuifunga gesti ni kutokana na ukaribu na shule,bei inayotozwa(1500/=) au maadili ya wanafunzi ni mabovu. Wasifurahi kufungwa kwa gesti tu kwani 'changes should start from within'. Wanafunzi wapenda ngono wote waache tabia hiyo mara moja kwani kwa bei ya 1500/= wanaweza wakaendelea kwenda gesti nyingine za jirani ambazo Kigogo,Luhanga,Manzese na Mburahati zimetapakaa.
   
 3. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Nimepokea habari hizi kwa furaha sana kwani: wanafunzi wa kigogo sekondari hawatafanya ngono tena, watakuwa na maadili mema, watasoma bila bugdha na watafaulu sana kwani kilichokuwa kinawafelisha kimeondoka-hongera wanafunzi wa kigogo seko.
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  halafu kuna bibi yuko hapo jirani kaambiwa ahamishwe, katuma ujumbe kwa jk anataka m 70! Sijui atazifaidi saa ngapi na umri ule
   
Loading...