Maisha ukiyajengea majibu chanya utakuwa na furaha siku zote!.
Mfano ukimpigia simu mpenzi wako asipopokea, JIPE JIBU KUWA "AMESINZIA" HATA KAMA NI SAA 5 ASUBUHI. Akikuta missed calls zako lakini akaghairi kukutafuta JIPE JIBU "HANA SALIO". Ukipiga tena ukakuta anaongea na mtu, JIPE JIBU KUWA ANAONGEA NA MZAZI WAKE hata kama ni usiku wa manane. Ukipiga tena akazima simu JIPE JIBU KUWA SIMU YAKE "IMEISHIWA CHAJI". Akiiwasha ukapiga akapokea akakujibu vibaya JIPE JIBU KUWA AMEKUMBWA NA "MSONGO WA MAWAZO". Jipe majibu mazuri siku ziende! Wewe endelea kujistresisha bila sababu!