THE POLITICA GAMBLE

Dr.adams faida

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
1,874
3,305
Katika SEASON ONE ya Series yetu iitwayo "The Political Gamble"...tayari nimemaliza kufanya upelelezi wangu wa Ki-nadharia juu ya wapi alipo kijana BEN...the investigation is 99 Percent Complete...na hii ni nadharia tu ila Practical itafanywa na Vyombo vya Usalama.

Mimi "P" a.k.a. Cuthbert Mtarimbo nachelea kusema yule kijana YU HAI....Swala la huko aliko atakuwa anakula BATA au MATESO sijui.

Huu ndio wakati ambao hashtag ya "BRING-BACK BEN ALIVE" ikiwa inatamba kuanzia kwenye Articles mpaka Tishrts sokoni.

"Nilifikiri kufa ni Tendo gumu,kumbe ni rahisi tu,laa matokeo ya kufa ndio Magumu, unaweza kumuua YERICKO hata sasa,Fikra zake hazifi (7:04 PM 15 sept 2015)

1f446.png
1f446.png
hiyo ni Tweet ya Mwisho ya Yericko tarehe 15 kabla ya kesho yake tarehe 16 sept 2015 kuripotiwa ametoweka...ametekwa...na kabla ya kubomoa kitu katika njia ya Uongo lazima ukijenge kidogo...Msingi hapa ulijengwa kwamba Yericko alichukuliwa Nyumbani na watu waliovaa sare za polisi halafu hakurudi....kwa mantiki hiyo hapa aliwahusisha polisi...Kumbuka Yericko na Ben ni Maswahiba wa kutupwa.

Sasa Campain ya "BRING BACK OUR YERICKO" ikawa kwenye chati kwa takriban wiki kadhaa huku ikisemekana katekwa au kauawa..but baadae akajitokeza tena mtaani shavu Dodo na ikadaiwa kwamba alikuwa busy na mambo ya familia..ikiwemo kupalilia Bamia zake kule Mbutu Kigamboni.....alikiri....Season 1 ikaisha.

SEASON 2 :
hapa tunamuona Mwanamama Salma Said akipotelea kisikojulikana wakati Uchaguzi wa Marejeo kule Zanzibar mwezi March 2016 hii ilikuwa Gumzo,... Ktk gumzo la kisiasa huku mitaani Prime suspect akawa yule yule...lawama pale pale, eti kwamba huyu Mama ametekwa kuzibwa mdomo asiripoti kinachojiri kwenye uchaguzi...sasa ikawa zamu ya Campain ya "BRING BACK OUR SALMA"...lakini baada ya siku 3 Salma akajitokeza hadharani akiwa ni mrembo zaidi ya mwanzo...uso wake ukimeremeta bila hata jeraha la Mbu huku yeye akipiga ngonjera ya kwamba watekaji walikuwa wakimtandika mateke usoni...sijui uso upi..hapa ikaonekana kwamba Mateke ya majasusi wale ni cute zaidi ya Dressing table za kituruki...hii Political Stunt ikakwama.....Season 2 ikaisha.

SEASON 3:
hii sasa inaitwa "BRING BACK OUR BEN ALIVE"...Prime Suspect amefanywa kuwa yule yule na watu wale wale,...inasemekana Ben katekwa....Ben haonekani Alipo..Lawama inatupiwa Serikali, the same situation kama ile ishu ya Yericko...je inatulazimu kuamini?..

Advocate Tundu amekuja na accusations zake..kwamba Ben kabla hajapotea alipokea ujumbe wa Simu ukimtia Mkwara Mzito juu ya namna gani anatakiwa kufunga Mdomo...Advocate Tundu anasisitiza kwamba baada ya kupata Message hiyo Ben ariripoti polisi....na hapa sasa ndio nakumbuka mwaka juzi namna nilivyovamiwa na Majambazi kule Tegeta halafu moja ya jambazi ndilo lilitoa Taarifa polisi kwamba nimevamiwa...polisi wakaja...majambazi yashakimbia...Jambazi mmoja akijibatiza jina la "Msamaria Mwema"
1f602.png


Huu ndio wakati sasa nikawa najiuliza how comes katika Digital World Watekaji watumie simu kutuma Message ya Mkwara kwa Ben huku wakijua huo ni moja ya Ushahidi?...kichwa kinauma...je ni namba ya simu inayotumika kwa muda mrefu au ilisajiliwa kwa lengo maalumu?..kwa kutumia GPS Vodacom wanaweza kutambua iliyokuwa Location ya mtumaji?

SEASON 4 ( Finale)
Nikumbushe tu kwamba Sterling hafi...Shujaa wa Season One amerudi tena kuhitimisha...Huyu ni YERICKO (The Man himself)...hapa sasa amesema atatumia siku 7 tu kwenda kumsaka na hata kumleta Ben aidha akiwa hai au mfu..kumbuka hawa ni Maswahiba wa kutupwa...Yericko sasa anarudi kule kule anapopajua kwenda kumleta Mwali wetu..its all Over..

Sasa Vyombo vya Usalama hapa ndipo pa kuambatana na kijana yericko awapeleke alipo mwenzake,he seems to know everything....je ni kwa style ipi Ben atatolewa mafichoni...hoja ipi itajengwa kutupoza sisi tuliolia mpaka kamasi?..wait n see.

[HASHTAG]#The[/HASHTAG] Political gamble
1f60e.png
 
Umeanza vizuri 2,ila mwishoni hapo nkajua unataka utuambie wapi Ben alipo...
 
Back
Top Bottom