The Official Azam FC Thread

[h=2]Tuesday, September 27, 2011[/h][h=3]MITIHANI MEMA HIMID MAO [/h]

Kiungo chipukizi wa Azam FC, Himid Mao ni miongoni mwa watahiniwa wa mwaka huu, ambapo wanatarajiwa kuanza mitihani yao hapo october 3.

Viongozi wa Azam Fans Club unamtakia mitahini mema Himid Mao pamoja na watahiniwa wengine na unamuombea dua afanye vyema katika mitihani hiyo ya kidato cha nne.

Mao ni miongoni mwa wachezaji walio ibuka kupitia Copa coca cola na kupata nafasi ya kujiunga na Azam Academy na kupandishwa katika kikosi cha Azam FC.

Himid Mao alikiongoza kikosi cha Azam Academy pale ilipotwaa Uhai Cup kwa mara ya kwanza katika msimu wa 2008/2009 na msimu ulio fuata alianza kupewa nafasi katika kikosi cha Azam FC.

Mao amekuwa kapteni katika timu za vijana za taifa kuanzia ile ya chini ya miaka 17 mpaka chini ya miaka 20.

Mitihani mema Himid Mao, twakungoja kwenye pitch baada ya kumaliza mitihani yako.

source: azamfans.blogspot.com​
 
MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Mrisho Ngassa, amefuata nyayo za mshambuliaji wa Arsenal, Robin van Persie, kwa kufunga bao la mapema zaidi kwenye mechi ya soka.

Ngassa ambaye alilifukuzia mbali jinamizi la ukame wa mabao kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kufunga kwenye mechi na JKT Ruvu, Jumamosi iliyopita, alifunga katika sekunde ya 36. Azam ilishinda mabao 2-0.

Bao hilo lilifananishwa na lile la Mholanzi Van Persie ambaye alifunga sekunde ya 27 wakati Arsenal ilipoiliza Sunderland mabao 2-1 katika Ligi Kuu England Jumapili.

Van Persie naye kama Ngassa, bado hajawaweza kuvunja rekodi za kufunga mabao ya mapema zaidi kwenye ligi zao.

Ngassa kwa mfano hajaweza kuvunja rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Boniface Ambani, ambaye alifunga katika sekunde ya 20 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika msimu wa 2008/09.

Pia Van Persie hajavunja rekodi ya beki wa Tottenham Hotspur, Ledley King, aliyefunga katika sekundi ya 10 dhidi ya Bradford mwaka 2000.

Ngassa aliyekuwa mfungaji bora msimu uliopita kwa kupachika mabao 16, angalau amepata bao la kwanza kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu.

Winga huyo anayeichezea pia timu ya taifa, Taifa Stars, alifunga baada ya kuwazidi ujanja mabeki, Damas Makwaya na Shaibu Nayopa, kabla ya kumtungua kirahisi kipa Shabaan Dihile. John Boko ndiye aliyefunga bao la pili dhidi ya JKT.

Ngassa sasa ameungana na washambuliaji KipreTchetche (Azam FC), Gervais Kago (Simba) na Mohamed Kijuso (Villa Squad) waliofunga mabao ya mapema msimu huu.
Naye kocha wa Azam, Stewart Hall, alisema baada ya pambano hilo kuwa amefurahi kumwona Ngassa akirejea katika makali yake ya ufungaji.
 
kikosi cha azam fc Mwidini, Erasto, Shikanda, Moradi, Aggrey, Mwaipopo, Sureboy, Jabir Aziz, Redondo, John Bocco na Ngassa.
 
Goooooooooooooaaaallll........ ni John Bogoooooli anafunga goli lake la 7 mpaka sasa Azam FC 2 Polisi Dom 0...
 
mpira umekwisha Azam FC 3 - 1 Polisi Dom
goli la tatu la Azam kafunga redondo..
 
zahoro.jpg
 
Kikosi cha leo dhidi ya Mtibwa Sugar Mwadini, Erasto, shikanda, Aggrey, moradi, mwaipopo, sureboy, jabir, Bocco, Ngasa and redondo
 
Back
Top Bottom