The Man in My dreams

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,265
Reaction score
4,453
Kuna mtu huwa kila mara ananitokea katika Ndoto

Huwa ananikatisha pale ambapo ninaongea na watu kuhusu mipango yangu.Huwa ananinyamazisha kwa ukali na kuniambia watu sio wema.

Mara nyingi ananitokea kwenye ndoto

Kiukweli mimi huwa na tabia ya kujadili au kuzungumzia mipango yangu na watu.Leo nimemkumbuka wakati wa mchana na sura imekuja kama vile ni mtu nimepata kumuona lakini nikijaribu kumkumbuka haji ispokuwa tu nimekumbuka maonyo yake yote aliyonipa.

Niulize wataalam wa mambo haya kama nilichukulie hili swala serious na niwe nakaa na mipango yangu moyoni bila kuwashirikisha watu

Nawakilisha
 
Aiseee,katika vitu vitakavyo kucheleweshea mipango yako ni hilo unalolifanya,.binadam sio wa kumshirikisha kila kitu,chagua mtu/watu muhimu kwako na sio kila mtu wa kumwambia au kumshirikisha unalotaka kufanya au unalolipitia...kuwa makini sio watu wote ni wema au wazuri..

Tena tuache kupuuzia ndoto tunazoota,zingine tunapewa ujumbe,lakini kwakuwa ni ndoto watu hupuuzia..
 
Mipango yako bora ufanye kimya kimya waone tu unafanikiwa

Binadamu wabaya,japo siyo wote,kuna baadhi yao ukiwaambia unakuta mipango haitimii miaka nenda rudi

Hivyo jifunze kuzuia ulimi wako,kuelezea mipango yako kwa watu,ukiacha utaona mafanikio
 
Unaongelea mipango yako kama njia ya kupata ushauri, kupata wabia au kujionesha?
ni vizuri hiyo ndoto ukaiishi ila kama unataka mbia, uwe mwangalifu ni nani wa kumweleza mipango yako.
 
Mi huwa sipuuzi ndoto naziheshimu sana na wewe mleta mada jifunze Kuwa na siri
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…