The Home Wrecker

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,531
Kun tatizo ambalo nimeliona sana kipindi hiki

Kuna mabinti wengi sana ambao wanaona ni sawa na kawaida kabisa kuwa na uhusiano na mume wa mtu na vijana ambao pia wanaona ni sawa kabisa kuwa na uhusiano na mke wa mtu.Tena kwa ujasiri kabisa wanasema kwaba WAKO IN LOVE

Hili swala limefanya nijiulize ni nini kinaendelea katika jamii yetu na mfumo wa malezi?Zamani mtu kuwa na uhusiano na mke/mume wa mtu lilikuwa ni jambo la aibu na lilifanyika kwa siri kubwa sana ila sasa hivi watu kabisa wanatunishia misuli wale wake au waume halali.

Imefikia mahali mpaka unashindwa kuelewa iwapo ni utamaduni au ni tabia ya mtu.

Mimi binafsi nimeshuhudia cases kama hizo na kuna binti ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 22 tu na TAYARI ameshazaa na waume za watu wawili,amevuruga Ndoa ninazofahamu mimi nne na nyingine zimeponea chupuchupu.Imefika wakati nikafikir huyu binti anamatatizo ya akili kwa sababu anapokuwa na mume wa mtu anakuwa na ujasiri wa ajabu sana(Anamfuata Mwanaume mpaka nyumbani kwake na kama akiona mke anammudu basi anajitambulisa kabisa kama mke mwenza.Ninajiuliza anapata wapi ujasiri huu?

Tujadili hapa ili kwa pamoja kuhusu hii tabia,sababu zake,madhara yake na namna ya kuirekebisha.
 
Ni sisi hao hao waume za watu tunaowafuata hao mabinti na kuwatongoza (tena kwa kuwahonga) vitu vya thamani kama vile pesa, gari na kadhalika.


Lakini ni hao hao wake za watu hujiweka katika mazingira ya kujirahisi (kujitongozesha) kwa vijana wadogo tena wakati mwingine kwa kuwarubuni kwa kuwahonga vitu mbali mbali kama vile kuwapa lifti katika magari yao, vyakula, vinywaji, nguo, saa, simu na kadhalika.

Fikiria; wewe ni mume wa mtu, unamtongoza binti kwa kumrubuni na vijihela vyako anakukubalia anakuvulia nguo unamlala mnaendeleza mahusiano hadi unampachika mimba. Hivi unategemea binti huyo ataacha kuwa jasiri juu yako? Keshakuona tupu yako, anakunyoa manywele yako huko chini , kuna nini hasa kitakachomzuia ashindwe kuwa jasiri???????!!!!!!!!

Haya mambo yalikuwepo tangu zamani isipokuwa kulikuwa na usiri sana kwa vile hakukuwa na huu utandawazi tulionao sasa. Matumizi ya mitandao yamekuja kuanika na kuyaweka wazi zaidi.

Ninao uzoefu mkubwa tu juu ya hilo. Shangazi yangu kabisa aliwahi kubadili nguo zake tumekaa sebuleni mimi, bibi na yeye. Katoka kuoga bafuni kaingia chumbani kwake katoka na mafuta na nguo za kubadilisha akatoa taulo lake akapakaa mafuta na kuanza kuvaa nguo mimi niko pale pale. Bibi alipojaribu kumhoji akamjibu kwani huyu sio mwanaume kama walivyo wengine? ana nini cha ajabu ambacho hakijui au mimi sikijui? Nikainuka nikaondoka zangu. Nilikuwa mtoto kwake yeye kwa maana ya kunizidi umri, lakini nilikuwa mtu mzima kijana mkavu kabisa niliyekwisha komaa.

Binadamu tuna tabia za mnyama yeyote unayemjua sema tumeumbwa na aibu ambayo unapokuwa faragha aibu hiyo hujificha. Tumeumbwa na tamaa.

Tueleze ukweli wako toka moyoni kama katika maisha yako hujawahi kuona mwanamke ukamtamani? Ni mara ngapi unaona mwanamke ukamfikiria ukamtamania kimyakimya lakini ukaishia kukaa kimyaaa?

Tupo baadhi ya watu ambao huona heri kula chakula kuliko kuwaka tamaa.

MUHIMU: Mke wa mtu ni sumu
 
Haya mambo ni magumu sana mkuu, na kwa mabinti/vijana wadogo kujihusisha na mtu aliye kwenye ndoa tena kwa ujasiri na kujiamini, kwangu mimi nadhani hili ni tatizo la kimaadili/malezi/makuzi.
Kimsingi uchepukaji wajati ukiwa kwenye ndoa sio jambo jema kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom