The Great Moshi Bank Heist, May 2004

The Great Moshi Bank Heist, May 2004

Texas Tiger

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2022
Posts
649
Reaction score
1,541
Ni asubuhi tulivu ya Ijumaa, Mei 21, 2004. Mji wa Moshi umeanza kuchangamka, watalii wanajiandaa kupanda mlima Kilimanjaro, wafanyabiashara wanafungua biashara zao, kila kitu kinaonekan kipo sawa. Lakini kule mtaani, kwenye Tawi la NBC Moshi, kuna mchezo mchafu ulikuwa unakaribia kuanza. Huu hukuwa ujambazi wa kishamba wa kuvizia watu ATM huu ulikuwa mpango wa "kisayansi" uliosukwa na vichwa hatari kutoka Kenya na wenyeji wa hapa nyumbani.

WASIFU WA MAJAMBAZI "THE DIRTY DOZEN"

Ili uelewe ukubwa wa tukio hili, lazima uwajue watu waliokuwa nyuma ya pazia. Hawa ndio "Main Actors" wa huu mchezo.
1. Wilfred Onyango Nganyi (The Mastermind)

Huyu ndiye alikuwa "Injini" na akili ya operesheni nzima. Raia wa Kenya mwenye asili ya mkoa wa Nyanza.

• Wasifu: Onyango hakuwa jambazi wa mtaani; alikuwa na uwezo mkubwa wa kupanga mipango (Strategic Planner). Alikuwa na rekodi ya matukio mengine ya ujambazi nchini Kenya na alijua jinsi ya kukwepa polisi kwa kutumia utambulisho bandia.

• Mchango: Yeye ndiye aliyetafuta "vifaa" (silaha na sare), aliratibu mawasiliano kati ya timu ya Kenya na wenyeji wa Tanzania, na ndiye aliyekuwa anatoa amri ya mwisho. Baada ya tukio, alikamatwa nchini Kenya akiwa na mali nyingi za kifahari.

2. Patrick Mutua (The Pro Driver)

Mkenya mwingine aliyekuwa na sifa ya kuwa na "moyo wa paka" anapokuwa nyuma ya usukani.

• Wasifu: Alijulikana kwa ujasiri wake wa kuendesha gari kwa kasi ya ajabu kwenye mazingira magumu (High-speed pursuit expert).

• Mchango: Yeye ndiye alikuwa dereva wa gari la kutorokea. Kwenye lile sakata la kufukuzana na polisi kuelekea Namanga, Mutua ndiye aliyekuwa anafanya "maneuvers" za hatari zilizowafanya polisi washindwe kuwapata kirahisi.

3. Jimmy Mzungu (The Enforcer)

Jina lake tu lilitosha kutetemesha watu. Mkenya huyu alikuwa na sifa ya ukatili na shabaha.

• Wasifu: Alikuwa ni mtu wa "Field". Alijua kutumia silaha nzito (SMG na AK-47) na hakuwa na huruma anapokuwa kwenye operesheni.

• Mchango: Alikuwa mstari wa mbele ndani ya benki. Yeye ndiye aliyekuwa anadhibiti usalama wa ndani (Crowd control) kwa kutumia vitisho na risasi. Alikuwa mmoja wa watu waliopambana na polisi kwa risasi wakati wanatoroka.

4. Simon Ndungu Mukono

Mshirika wa karibu wa Onyango na mmoja wa watu walioingia ndani ya benki.

• Wasifu: Jambazi mzoefu wa mipakani aliyekuwa anajua vizuri njia za "panya" za kuvuka kutoka Tanzania kwenda Kenya bila kupita uhamiaji.

• Mchango: Alisaidia katika uratibu wa kutoroka na kuhakikisha mzigo (fedha) unafika Nairobi salama.

5. Boniface Anyanzwa (The "Bishop")

Boniface alikuwa akijitambulisha kama kiongozi wa dini (Askofu) nchini Kenya.

• Wasifu: Alitumia kivuli cha dini na kanisa lake kuficha uhalifu. Alionekana kama mtu mwenye heshima katika jamii yake Nairobi.

• Mchango: Alishitakiwa kwa kusaidia kuficha majambazi hao baada ya kutoroka Tanzania na kusaidia katika utakatishaji wa fedha (Money Laundering). Alitumia nyumba yake na majengo ya kanisa kama "Safe Houses" kwa ajili ya Onyango na genge lake.

Mbali na hao "Big Five", kulikuwa na watu wengine waliohusishwa kwa kutoa taarifa, kusaidia usafiri au kuficha mali.

1. Samwel Githinji Njau: Mkenya aliyekuwa sehemu ya kikosi cha mashambulizi.

2. Michael Joseph Mbanya: Mwingine aliyekuwa kwenye "Field Team".

3. Gabriel Gathua Chege: Alihusika katika maandalizi ya awali ya kijasusi (Reconnaissance).

4. Grace Kagure Ng’ang’a: Alihusishwa na masuala ya kutoa hifadhi na usafiri kwa majambazi hao nchini Kenya.

5. Gabriel Kariuki: Mmoja wa watu waliokamatwa katika msako mkali nchini Kenya na kurudishwa Bongo.

6. David Ngugi: Alihusishwa na uratibu wa mali zilizopatikana kutokana na wizi huo.

7. Juma Ramadhani (Mwenyeji): Huyu alikuwa mtanzania aliyesaidia kutoa taarifa za mazingira ya Moshi na ratiba za benki (Inside job informant).

8. Lucas Mmari: Mtanzania mwingine aliyedaiwa kusaidia katika masuala ya vifaa na maficho ya awali kabla ya kuvuka mpaka.
MCHONGO ULIVYOKUWA.

Majira ya saa 2:30 asubuhi, gari jeupe aina ya Land Rover Defender, likiwa na nembo za kampuni ya ulinzi ya Ultimate Security, liliingia ndani ya uzio wa benki. Walinzi wa benki, wakiwa wamejawa na nidhamu, walifungua geti kwa tabasamu wakidhani ni wenzao.
Sekunde chache baadaye, milango ya gari ilifunguka kwa kishindo. Watu wenye maski nyeusi na sare za ulinzi waliruka nje. Lakini mkononi hawakuwa na vitambulisho, walikuwa na AK-47 na SMG. Mlinzi mmoja alijaribu kuinua bunduki yake—hakupewa nafasi ya pili. Risasi ya kwanza ilipasua kichwa chake, na ya pili ilimpiga kifuani mlinzi mwingine. Walidondoka hapo hapo, damu yao ikitapakaa kwenye sakafu ya benki. Ndani ya benki, kelele za "Lala chini! Lala chini!" zilizizima. Wateja walijitupa sakafuni, wengine wakikojoa kwenye suruali kwa hofu ya kifo.
Majambazi walielekea moja kwa moja kwenye Strong Room. Walipakia magunia ya fedha—Tsh Bilioni 5.3! Pesa za Kitanzania, Dola, na Euro zilijazwa kwenye gari kama magunia ya mahindi. Ndani ya dakika 15 tu, mji wa Moshi ulikuwa umeanza kuzizima kwa milio ya risasi.

KUTOROKA.

Baada ya kupata "ganji", Patrick Mutua alikanyaga mafuta. Land Rover ilinguruma na kutoka nje ya benki kwa kasi ya ajabu. Polisi wa Moshi, wakiwa wamechelewa kidogo, walianza kuwafukuzana nao kwa magari yao ya doria. Haikuwa mbio ya kawaida ilikuwa ni vita. Majambazi walikuwa wanachungulia kwenye madirisha ya gari na kumwaga risasi za mfululizo kuelekea magari ya polisi. Barabara ya kuelekea Arusha iligeuka kuwa uwanja wa vita. Raia waliokuwa wakielekea kazini walilazimika kuacha baiskeli na magari yao na kujitupa mitaroni huku risasi zikipita juu ya vichwa vyao. Walipofika kwenye vizuizi vya polisi (Roadblocks), majambazi hawakupunguza mwendo. Walikuwa wanapita katikati ya vizuizi huku wakimwaga "mvua" ya risasi. Walifanikiwa kuwaua askari wengine na raia wasio na hatia waliokuwa wamepata mkosi wa kuwa njiani wakati huo. Kwa kutumia njia za panya walizokuwa wamezichora mapema, walifanikiwa kuingia maporini, wakavuka mpaka wa Namanga na kuingia nchini Kenya.

KUKAMATWA: MSAKO WA INTERPOL NA USALITI WA PESA

Wakiwa Nairobi, genge hilo lilianza kuishi maisha ya kifahari kama wanavyofanya wahalifu wote. Wilfred Onyango na wenzake walianza kununua majumba ya kifahari, magari ya "zero kilometer" na kuanza kufanya anasa ambazo raia wa kawaida angeweza kuziota tu.
Lakini walisahau jambo moja, damu haina siri. Polisi wa Tanzania na Kenya chini ya mwavuli wa Interpol, walianza msako wa kimya kimya. Walikuwa wanazifuatilia zile fedha. Majambazi walianza kusalitiana wenyewe kwa sababu ya tamaa. Mmoja baada ya mwingine alianza kunaswa. Wilfred Onyango alikamatwa akiwa amejificha Nairobi. Kurudishwa kwao Tanzania (Extradition) kulikuwa ni vita nyingine ya kisheria. Mawakili wao nchini Kenya walipambana kuzuia wasiletwe Bongo wakidai watateswa, lakini serikali ya Tanzania ilisimama kidete. Walirudishwa nchini chini ya ulinzi mkali wa makomandoo, huku pingu zikiwa mikononi na miguuni.

MAHAKAMANI: VITA YA MAWAKILI

Kesi hiyo ilidumu kwa miaka 10, mwaka mmoja kwa kila mmoja wa wahusika wakuu. Mahakama ya Moshi ilikuwa inafurika kila siku. Mawakili wa utetezi walijaribu kutumia mbinu zote za "Kiingereza cha kisheria" "Mheshimiwa Jaji, wateja wangu hawajakamatwa na ushahidi wowote wa kisayansi. Hakuna DNA, hakuna alama za vidole. Hii ni kesi ya chuki tu dhidi ya Wakenya waliofanikiwa!"

Lakini Upande wa Jamhuri, ukiwa na mawakili mahiri, ulileta mashahidi 32. Walionyesha risiti za magari, walileta rekodi za simu zilizowaunganisha wote 13 kuanzia siku ya kwanza ya mchoro hadi siku ya kutoroka. Walileta picha za maiti za walinzi, jambo lililofanya ukumbi wa mahakama ujawe na simanzi.
Mnamo mwaka 2014, Jaji alisimama kutoa hukumu. Alisema kuwa huu ulikuwa ni unyang'anyi wa kikatili uliopangwa kwa makusudi. Nyundo iligonga meza. Miaka 32 jela kwa kila mmoja wa viongozi wa genge hilo. Mali zao zote nyumba, magari na fedha zilizobaki zilitaifishwa na serikali ili kufidia pengo la NBC.

Leo hii, Wilfred Onyango Nganyi, Patrick Mutua na washirika wao wametungwa gereza la Karanga, Moshil
 
Aisee km movie vile ila ungeanza nyuma kidogo umeanzia katikati sana, yaan kabla kuanza kupiga tukio
 
Back
Top Bottom