The Electronic and Postal Communications Act, 2010 ndiyo inatumika Vodacom kutoa taarifa mahakamani

SirBonge

JF-Expert Member
Jul 18, 2010
378
435
Sheria hii 99 (a) ndio iliyotumika kwa VODACOM kutoa taarifa za washitakiwa. Suala kwamba Staff wa VODA anasimama mahakamani au wanatoa tu taarifa za maandishi, sidhani kama ni la muhimu, Offcourse kama Mahakama imewataka watoe pia Ushahidi wa mdomo, ni Lazima wafanye hivyo. WaTZ tupunguzeni mihemko, tuwe tunajisomea kidogo kabla ya kulaumu vitu

upload_2017-1-21_2-13-10.png
 
View attachment 462059
Mkuu Sir Bonge, Asante kwa hii kitu.

Paskali
 
Watu umefika muda wakubali tu kuwa jamaa alikosea basi huku kuwalaumu Vodacom wakati kila kitu kipo wazi hakusaidii kitu.

Wengine wajifunze, siasa za kutukanana hazina manufaa kwetu.
Mbona mkapa aliwatukana watanzania ni wapumbavu tena malofa.
 
Watu umefika muda wakubali tu kuwa jamaa alikosea basi huku kuwalaumu Vodacom wakati kila kitu kipo wazi hakusaidii kitu.

Wengine wajifunze, siasa za kutukanana hazina manufaa kwetu.
Nashangaa kinachowauma.kwani.mitandao.ni Voda peke.yake??Tupo na Halotel
 
Sheria hii 99 (a) ndio iliyotumika kwa VODACOM kutoa taarifa za washitakiwa. Suala kwamba Staff wa VODA anasimama mahakamani au wanatoa tu taarifa za maandishi, sidhani kama ni la muhimu, Offcourse kama Mahakama imewataka watoe pia Ushahidi wa mdomo, ni Lazima wafanye hivyo. WaTZ tupunguzeni mihemko, tuwe tunajisomea kidogo kabla ya kulaumu vitu

View attachment 462059
tatizo la ushahidi wa sms hauthibitishi kamwe ni nani aliutuma hasa katika ngwe hii ya hackers kwa hiyo huwezi kuthibitisha kama mshtakiwa ndiye aliyetuma na kufanya hicho kifungu kuwa na maana kwenye voice data tu na wala siyo written data. Mbaya zaidi kwa watumishi wa makampuni ya simu hawana utaalamu wa kutambua sauti na hivyo ushahidi wao hata kwenye voice data kuwa hauna maana na kufanya hicho kifungu cha 99(a) kuwa hakitekelezeki
 
tatizo la ushahidi wa sms hauthibitishi kamwe ni nani aliutuma hasa katika ngwe hii ya hackers kwa hiyo huwezi kuthibitisha kama mshtakiwa ndiye aliyetuma na kufanya hicho kifungu kuwa na maana kwenye voice data tu na wala siyo written data
Ni sawa mkuu, lakini cha kwanza ni kuthibitisha kwamba ujumbe ni kweli ulitumwa jutoka kwenye simu ya mtuhumiwa. Na hichi ndio VODA watakachofanya. Suala la nani alituma toka kwenye simu ya mtuhumiwa linahitaji ushahidi mwingin. Lakini anayekutwa na ngozi si ndio muiba g'ombe! Hata kama sio yeye atamjua aliyeiba....kwa hiyo ataisaidia mahakama...tafakari.
 
Mkuu Sir Bonge, Asante kwa hii kitu.

Paskali
Kesi hii inahusu tusi kwa mtu..ni tort hivyo adhabu yake ni fidia kwa mwathirika hivyo not a big deal.sidhani ukimpiga mtu au kumtukana basi kuna kifungo. Kama zipo adhabu hizo katika sheria zetu basi zina matatizo. Maana haina mantiki Pascal anivunje mkono halafu atupwe jela ...jee hio ndo remedy kwa mkono wangu?
Adhabu ni kumuamuru mkosaji alipe fidia na ndio kesi hii ya lema na mkewe.
Hivyo hata voda wakitoa ushahidi basi madam matusi hayo hayakuwa public mahakama inaweza hata kumuamuru lema kumuomba radhi tu mhusika. Sio kesi ya kukaa na kupoteza fedha bure
Ila kama ni mtaji wa kisiasa thn gharama sio muhimu.
 
Mkuu Marcos ni kweli kumtukana mtu ni tort ila pia kuna kitu kinaitwa "criminal trespass" ukituma sms ya kutishia kuua" sio tort ni criminal.

Mfano kila binadamu kuna siku lazima atakufa, hivyo nikituma SMS kusema "Marcos Utakufa!" sio kosa, kwa sababu ni kweli kuna siku Utakufa, ila nikisema "Marcos utakufa kabla ya 2020" ni sawa na kusema "nitakuua kabla ya 2020" hii ni criminal trespass.

Paskali
 
Vodacom si wakulaumiwa, wa kulaumiwa ni hawa wanaotaka taarifa za tena taarifa zao wanatakaga wanazopenda wao tu.

Suala la ULIMBOKA sikuona kwann Polisi hawakuhitaji ushahidi suala la Ben SAA 8 sijui kwann hawakuhitaji ushahidi.

Na kibaya zaidi Mke wa Lema anakiri kuwa alimtext Gambo hiyo sms so ushahidi upi wanaoutoa ilihali mtuhumiwa kashakiri kutuma hiyo SMS.

Watafsiri tu hiyo SMS kama ni kosa kuliko kutaka ushahidi.. Ambao tayari wanao
 
Sheria hii 99 (a) ndio iliyotumika kwa VODACOM kutoa taarifa za washitakiwa. Suala kwamba Staff wa VODA anasimama mahakamani au wanatoa tu taarifa za maandishi, sidhani kama ni la muhimu, Offcourse kama Mahakama imewataka watoe pia Ushahidi wa mdomo, ni Lazima wafanye hivyo. WaTZ tupunguzeni mihemko, tuwe tunajisomea kidogo kabla ya kulaumu vitu

View attachment 462059
Umesomeka mkuu
 
Ninachofahamu VODACOM au kampuni yoyote ya simu hairuhusiwi kutoa mawasiliano ya simu pasipo amri ya mahakama. Nafikiri itakuwa si sahihi kuilaumu Vodacom kwa sasa wakati wala hatujui aina ya ushahidi wanaokwenda kuutoa. Je kama wameitwa kuthibitisha usajili wa hiyo laini bado tutasema wametoa siri za mteja?
 
Back
Top Bottom