jerrytz
JF-Expert Member
- Oct 10, 2012
- 5,975
- 4,264
Jumuiya ya wanasheria wa Afrika Mashariki (The East Africa Law Society) imelaani na kuhuzunishwa/kusikitika na kutounga mkono kauli ya Waziri Katiba na Sheria wa JMT Dr.Harrison Mwakyembe kuhusu kuifuta Tanganyika Law Society kama jumuiya hiyo itajiingiza katika harakati za kisiasa.
Mwakyembe ambaye pia ni Mwanasheria alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa jumuiya hiyo itafutwa iwapo itajihusisha na harakati za kisiasa.
East Africa Law Society iliweka wazi kupinga,kulaani na kutokukubaliana na vitisho hivyo katika barua wazi iliyomwandikia Mh. MWAKYEMBE ikiwa na kichwa kinachosomeka "BARUA YA WAZI JUU YA VITISHO KWA UWEPO WA TANGANYIKA LAWSOCIETY"
Barua ambayo imesainiwa na Rais wa EALS Richard Mugisha imeeleza kuwa matamshi ya waziri vitisho vibaya kabisa kwa kanuni za uhuru kwa katika fani ya sheria.
Barua hiyo inasomeka zaidi " uhuru wa wanasheria ni kanuni ya msingi wa sheria za kimataifa ambayo imeimarishwa kwa maazimio na makubaliano ya kikanda na kimataifa ya Umoja wa Mataifa (UN) ambapo Tanzania imeridhia maazimio hayo. Hivyo basi tunamuomba Mheshimiwa Waziri asome na kutakari juu maazio hayo ambayo Serikali ya Tanzania imeyasaini na kuhakikisha kwamba yanaheshimiwa. Kuifungia TLS ni kukandamiza utawala wa sheria"
Nawahi kibaruani kwa habari zaidi soma The Guardian 23rd