Tokea aingie madarakani rais Magufuli amekuja na style yake mpya ya utawala wake wa kutumbua majipu kiasi kwamba amejizolea sifa nyingi sana hapa nchini na nchi za nje.Kuna baadhi ya mambo mazuri ameshafanya kwenye siku 100 tokea aingie ofisini .
Pia kuna masuala mengine yametendeka na kugubikwa na sintofahamu miongoni mwa wananchi katika siku zake hizo mia moja za ofisini.
Nataka nizungumzie suala la demokrasia ,katika suala hili naona Rais Magufuli ana walakini katika hili la kipengele hichi cha demokrasia. Katika hotuba yake ya awali aliwahi kusema uchaguzi umekwisha sasa tujenge nchi na mimi ni rais wa watu wote huku akiwalenga wapinzani.
Kuna suala la uchaguzi wa Zanzibar hili analijua wazi na lakini anajifanya halijui na hahusiki nalo kiasi kwamba jumuiya za kimataifa wanalifuatilia kwa ukaribu sana .Huku akiwatisha wa Zenj kwa nguvu za kijeshi.
Kitu kingine ni uchaguzi wa mameya katika baadhi ya miji, tumeona figisu figisi zinazo tokea kwani chama chake hawakubali kushindwa kwenye masanduku ya kura ingawaje wananchi wamewakataa.
Mimi naamini utawala bora wa kiongozi yeyote ule katika nchi huendani na demokrasia na sio vitisho kwa wapinzani sabubu kuna mambo mazuri serikali inaweza kuyachukua toka kwa wapinzani katika shughuli za kuongoza nchi.