The committee of 300

Si kweli,Shetani amekudanganya.Kambi ziko mbili,ya Shetani na Mungu,the almighty.Shetani hawezi kufunua uovu wake,ni kambi ya Mungu tu inayoweza kufunua uovu wake.It's common sense,ufalme ukijifitini hauwezi kusimama.


Hawatakuelewa ni ngumu mtumishi 1kor 2:11-16. Zaidi sana sana utaishia kuraruriwa Mt 7:6
 
Kiukweli maswali yako ni ya msingi na yana hoja, ila wangekuwa wanajitokeza kuyajibu ingefaa zaidi. Mimi ntakujibu kadhaa , kuhusu tawala za kirumi n.k hizo zilikuwa ni tawala za kifalme ambazo mtu mmoja anafanya maamuzi kutokana na matakwa yake, katika serikali moja ya ulimwengu, hapa maamuzi yanatokana na wanachama wote, na siyo serikali ya mtu mmoja au nchi moja.

Kuhusu silaha za maangamizi, hizo zitaendelea kuwepo,ila zitapunguzwa na itakuwa ni rahisi kuendesha uzalishaji na usimamizi wa hizo silaha.

Kuhusu umasikini, inawezekana kuutokomeza au kuendelea kuwepo, vyote inawezekana, ila utaweza kupungua kwa kiasi chake kwa sababu mifumo ya uendeshaji wa serikali za nchi itakuwa centralized, kwahiyo itakuwa ni rahisi kutekeleza na kutimiza mikakati ya kupambana na umasikini.

Kuhusu uwajibishwaji wa serikali, inaweza kuwepo katiba bora, ambayo itatoa mwongozo juu ya uwajibishwaji wa hiyo serikali endapo itaenda kinyume na katiba.

Kuwepo kwa Jeshi moja, itasaidia kuyadhibiti majeshi mengine yanayofanya uasi na kuyadhibiti majeshi ya ndani ya nchi yasilete mapinduzi. Kwa kuangalia mifano ya serikali ya USA, Chini na Russia, ambayo ndani yake kuna visiwa na baadhi ya mamlaka za serikali ambazo zinajiendesha zenyewe ila zipo chini ya usimamizi wa serikali kuu na hatujaona zimerudi nyuma kimaendeleo bali zinazidi kuchanja mbuga, hata hili la serikali moja ya ulimwengu linawezekana.

Hata Afrika tungekuwa na serikali kuu moja tungekuwa mbali kimaendeleo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…